Monday, May 16, 2011

Majibu ya MMILIKI WA TUZO ZA BLOG TANZANIA

Hivi karibuni niliandika kuhusu Tuzo za Blog Tanzania na kutoa MTAZAMO NA MSIMAMO WANGU (hapa) na sasa mmiliki / mwongozaji wa blogu inayotayarisha tuzo hizo amejibu kuhusu mtazamo wangu. Nami napenda kuweka maoni yake hapa
FRIDAY, 13 MAY, 2011
Admin said...
Wow! Nilikua sijapata muda wa kusoma link ulizoacha kwenye blog yetu. Leo ndio nimepata muda nimepitia huku sasa hivi ndio nikaona umeandika maoni yako kuhusu tunzo yetu. Kwanza nikupe shukurani kwa vile kuandika post kuhusu kitu fulani sio jambo dogo..

Ila ninalotaka kusema ni kuwa kila mtu anaruhusiwa kutoa mawazo yake na kueleza jinsi anavyofikiria. Sasa na mimi kwa upande wangu naweza nisikubaliane na hata kitu kimoja unachosema au nikubaliane na vichache tu.

1.Unavyosema la muhimu ni kuwa na umoja wa wanablog kwanza sikuelewi una maana gani. Unajua umoja wa kitu chochote haulazimishwi? Na kila mtu au watu wanaojiunga katika umoja fulani ni kwa kutokana na jinsi wanavyoona huo umoja utawasaida vipi kutokana na kanuni za umoja huo. Wanawake fulani wakikaa wakaamua waanzishe umoja wa wanawake wanaoblog, je utamlazimisha kila mwanamke anayeblog ajiunge na umoja huo? Kama hataki je watu waliokua kwenye umoja huo watamfikiriaje mtu ambaye hayupo kwenye umoja huo? Je watamtenga, watachukia blog yake, watafikiria kuwa anajiona yeye yuko juu zaidi kuliko wale waliojiunga kwenye huo umoja au waanzilishi wa huo umoja? Hivyo sioni sababu ya kulazimisha kuanzisha umoja wowote kama watu hawako tayari au hawajui umuhimu wa umoja fulani. Ujue kuwa umoja wowote unaoanzishwa iwe kwenye nchi, makazini, kwenye makanisa au misikiti ni kwa manufaa ya wanachama kama sivyo basi hauna maana. Na mimi ninavyofahamu kuna kundi la watu wanaokutana jijini Dar Es Salaam kujadili blog zao kila mara. Sasa hilo kundi sijui nao utawaambia kwanini mnakusanyika wenyewe bila kutangaza au kutwambia na sisi tujiunge? Hivyo umoja unaouzungumzia si ajabu upo lakini ni kwa watu fulani. Hivyo na wewe unaweza ukaanzisha umoja na kuutangaza humu na kueleza madhumuni na faida za umoja huo ili wenye kuona unawafaa wataamua kujiunga au la. Usikae na kuimba wimbo wa “tuanzishe umoja, tunzishe umoja” tu. Wewe kama mwana blogger unatakiwa ndio useme jamani nimeanzisha umoja huu, madhumini yetu ni haya na kanuni zetu ni hizi hivyo mwenye kutaka kujiunaga atajiunga.

2.Halafu unavyosema kabla ya tunzo kwanza tufundishane umuhimu wa blog kwa jamii…Sasa kama ni hivyo Oscar awards ambayo ni tunzo ya juu sana katika ulimwengu wa filamu nao wasingeanzisha hiyo tunzo mpaka leo wakisubiri watu wafahamu umuhimu wa filamu katika jamii. Hivyo hilo sitakubaliana na wewe pia kabisa kwa vile mpaka leo kuna filamu hazina maudhui yeyote katika jamii zaidi ya kufurahisha tu. Na hilo utalikuta kwenye blog nyingi tu, sio zote zitakua za kufundisha jamii kuna blogs ambazo zitakua zinafurahisha tu lakini zote zitashirikishwa katika mashindano. Na ni juu ya waanzilishi wa Oscar awards kuchagua ni filamu gani wazishirikishe na gani wasizishirikishe. Hawalazimishwi na watu wa filamu. Watu wa filamu ndio wanajitahidi kutengeneza filamu zao kwa ubora zaidi ili zitambulike humo. Na sisi hapa hatutalazimishwa na mtu yeyote ni wajibu wetu kuiweka award yetu katika kiwango cha juu. Na uzuri wa award yetu ni kuwa watu wanaosoma hizi blogs ndio watakao chagua wenyewe. Tumeshazoea kuona vyombo vya habari vinavyojua kumpalilia mtu kwa vile ni fulani au anajulikana na watu fulani kuliko mtu mwingine anayefanya mengi lakini kwa vile hamjui yeyote yeye jina lake halipitishwi mahali popote. Hayo yapo sana tu lakini hapa kwetu ni people’s choice hata yule mtu ambaye amejitahidi sana kujitangaza na hakuonekana tunampa jukwaa la kuonekana.

3. Na unavyosema sijui tuwaandikie watu watueleze blog zao zinahusu nini. Kwa taaarifa yako kuna watu wengi wanablog lakini hawajui hata blog zao zinaelekea wapi. Kuna maswali tumetuna na kuna wengi wamesharudisha lakini nakwambia ni kama 50% ya waliorudisha mpaka sasa hivi hawajui blog zao zinahusu nini au wasomaji wa blog zao ni nani. Mtu anaweza kuwa na mawazo yake fulani lakini kile anachokichapisha kwa watu ni tofauti kabisa na kuna wengine kwa kufuata mkumbo wa huku na kule basi waliloanza nalo sio lile wanalo sasa hivi. Hivyo baada ya watu kuwakilisha blog zao tutakaa chini kuona kama kila blog iliyopitishwa inastahili kuwekwa katika hiyo category.
SUNDAY, 15 MAY, 2011

KISHA AKAENDELEA
Admin said...
Halafu ukishapangia watu nani apewe tunzo ya juu na nani anastahili zaidi kuliko mwingine hiyo si sawa kabisa. Kila mtu anayefanya jambo lolote linalosaidia jamii kwa njia moja au nyingine anastahili pongezi. Kuna watu wengi sana wanatoa michango yao katika jamii lakini labda kwa vile uwezo wao ni mdogo basi michango yao haisikiki au haifiki katika ngazi za kitaifa nao ikifika siku ya kutambuliwa utawapengua na kusema nyie hamstahili kwa vile mmesaidia huko vijijini tu na wala sio zaidi? Ina maanisha kama mtu amesaidia kuokoa maisha ya mtoto aliyekua afe huko kijijini na mtu aliyesaidia maisha ya mtoto aliyekua afe mjini ni yupi anastahili pongezi zaidi? Je wanatofauti hao watu katika ustawi wa jamii? Ndio maana kuna awards na life time achievement awards nadhani unaelewa tofauti kati ya hayo mawili. Award inapigiwa kura lakini life time achievement awards inateuliwa. Kama ingekua hapa tunachotoa life time achievement award na wewe ukapendekeza jina la mtu fulani ningekuelewa vingine sitakuelewa au nitaanza kufikiri au una agenda fulani. Kuna watu wanastahili tunzo ya life time kwa michango yao wameitoa kwa muda mrefu katika jamii lakini usimkatishe tamaa yule mtu anayeanza tu kutoa mchango wake katika jamii kwa kutomtambua au kwa vile hana zana wala uwezo wa kufanya makubwa ili taifa kumtambua mchango wake. Hata kama ni mchango wake ni mdogo tu unaoishia katika kijiji chake anastahili pongezi sawa kama yule mwenye uwezo na kufanya mambo makubwa zaidi. Watu wote wanaofanya jambo lolote kwenye jamii linalosaidia kuboresha ubora wa maisha ya watu wanastahili kutambuliwa na kupongezwa.


Lingine ni lile ulivyosema tuwekeze “kuhamisha maandiko yetu kutoka kwenye blogu kuelekea kwenye MAGAZETI yanayosomeka na wengi” . Hapa sikubaliani na wewe kabisa. Cha muhimu ni vyombo vya habari kuhakikisha kuwa wanaweka habari zao kwenye mitandao kwa vile kuna watu wengi wako nje ya nchi na wana kiu za habari za nyumbani na wahazipati hivyo ndio maana unaona blog za bongo nyingi ni za habari tu kwa vile ndio wanaona kuna watu wengie wanakimbilia huko. Either walio bongo wanataka habari za nje ya nchi na walio nje ya nchi wanataka habari za bongo. Kwa kusema tutafute njia ya kupeleka blog kwenye magazeti unatakiwa kujua kuwa kila nchi inasheria zake za uhuru wa habari. Na kila gazeti linasimama kufuata sheria za nchi na sheria za malengo ya magazeti yao. Magazeti kama sio ya serikali basi hufanya kazi kwa ajili ya biashara tu. Usitegemee gazeti la watu binafsi liko kwa ajili yako liko kwa ajili ya kuchapisha habari itakayouza gazeti lao na kupata faida. Hivyo hata kama kuna vitu watu wanatuma viwekwe kwenye magazeti lakini haviweki kwa ajili labada ya kanuni zao, hazifikii ubora wa habari zao au kwa sababu zao nyingine. Hivyo ukisema kila linalokua blogged na watu huku kwa vile unafikiria ni bora basi linahitaji kusomwa na wale hata wasiokua na uwezo wa kuingia kwenye mitandao inaweza ikawa n vizuri lakini sio kila blog ina maudhui. Sasa kila kinachowekwa kwenye blog kikiwekwa kwenye gazeti patakalika kweli. Cha muhimu ni wewe kama una mawazo hayo basi anzisha kitu kama blog magazine na uwe unachapisha blog yako au post za blog za watu wengine ambazo unaziona ni muhimu kwa kujenga taifa lakini nafahamu baada ya muda ili kuuza gazeti lako hata wewew utakua unachapisha vitu unavyoona vinauza gazeti lako tu. You know that is the way life is….wengi huwa wanaanza kwa madhumunimazuri lakini baadaye wanakua greedy na kusahau maadili ya biashara zao…Na pia ukumbuke kila nchi ina sheria zake za mambo ya habari. Ndio maana kuna email ya mtu ambaye aliishi Tanzania na kuweza kufahamu lugha ya Kiswahili. Katika pita pita akaona hii tunzo yetu na alifurahi sana kwa vile huko nchi yake aliko wao kwa bado hawawatambui hii kabisa na wau wanaoblog wanachukiwa sana tu na hata na serikali. Hivyo hata sisi nchini kwetu sidhani kuwa kuna gazeti litaweza kusurvive hata mwenzi mmoja likiwa linahapisha baadhi ya topics zinazowekwa humu kwenye blogs…
SUNDAY, 15 MAY, 2011

Ndugu yangu ADMIN......Kabla sijaendelea na yangu wacha nikupe ya wenzangu ambao kwa bahati mbaya maoni yao yalifutika kutokana na tatizo la BLOGGER juma lililopita, lakini bado yapo kwenye email


Mfalme Mrope has left a new comment on your post "TANZANIAN BLOG AWARDS...Mtazamo na msimamo wangu":

nani yuko kwenye kamati ya kuteua hizi blogs na ni nani mpiga kura na pia mpendekezaji ni nani na tangazo la hii kampeni lilitolewa lini? na ati? Michuzi iko kwenye best designed blogs?? HUH?
Posted by Mfalme Mrope to "The Way You See The Problem Is The Problem" at Wed, May 11, 2011 at 11:23 PM

Yasinta Ngonyani has left a new comment on your post "TANZANIAN BLOG AWARDS...Mtazamo na msimamo wangu":

nanukuu.."NA HIVI NDIVYO NIONAVYO TATIZO, LABDA NAMNA NIONAVYO TATIZO NDIO TATIZO" mwisho wa nukuu. haswa ni tatizo.
Naungana na kaka Mrope nani alipiga kura? na nani aliamua kila kitu?...
Posted by Yasinta Ngonyani to "The Way You See The Problem Is The Problem" at Thu, May 12, 2011 at 3:21 AM

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) has left a new comment on your post "TANZANIAN BLOG AWARDS...Mtazamo na msimamo wangu":

Mimi nilipoona tangazo hili wala sikutaka kusema cho chote. Ingekuwa vizuri hao waandaaji wakajaribu kuwasiliana na wanablogu wote ili tukashirikishwa.

Mzee wa Changamoto: Hakikisha post hii inawafikia hao waandaaji. Ingekuwa vizuri kama nasi wanablogu tulioko nje tukashirikishwa. Mimi binafsi ningependa kuona vigezo vinavyotumika katika uteuzi. Asante sana kwa kuliona hili.
Posted by Masangu to "The Way You See The Problem Is The Problem" at Thu, May 12, 2011 at 9:02 AM

Malkiory Matiya has left a new comment on your post "TANZANIAN BLOG AWARDS...Mtazamo na msimamo wangu":
- Hide quoted text -

Yaelekea bloggers wa kitanzania tuishio nje tumeshapokonywa uraia wetu na waandaaji wa tuzo hii. Inashangaza kuona blogs ambazo ni chachu katika kuelimisha watanzania popote pale duniani, ndizo zimepigwa chini. Na zaidi ya yote zile blogs ambazo hufanya uchambuzi yakinifu katika masuala ya siasa, utawala bora nazo zimepigwa chini. Kuna kila sababu ya kutilia shaka Lengo, nia, madhumuni na vigezo vya tuzo hii.
Posted by Malkiory Matiya to "The Way You See The Problem Is The Problem" at Thu, May 12, 2011 at 1:14 PM

NITAENDELEA NA MAONI YA KWENYE FACEBOOK BAADAE.
Lakini kama nilivyosema katika POST YENYEWE, kwamba 'NDIVYO NIONAVYO TATIZO....NA LABDA NAMNA NIONAVYO TATIZO NDILO TATIZO'

5 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

http://kamalaluta.blogspot.com/2011/05/wanaotoa-tunzo-za-bloggers-na-watoe-kwa.html

Unknown said...

http://mtayarishaji.blogspot.com/2011/05/majibu-ya-mmiliki-wa-tuzo-za-blog.html

malkiory matiya said...

Huyu jamaa wa tuzo ya blogs naona ametoa majibu mepesi sana. Kila mtu katika dunia hii anao uhuru wa kufanya kile apendacho. Kwahiyo ninachotaka kusema hapa ni kwamba si kazi yake kukosoa watu kuwa wanafuata mkumbo. Kwa jinsi alivyojibu inaonesha kwamba yeye tayari alishapanga matokeo mezani.

Kati ya blogs zilizokwisha orodheshwa hadi sasa bado sijaona blogu zilizoenda shule kama vile . WAVUTI, MATONDO, CHAHALI, MHANGO, MUBELWA, MBELE, KITURURU, CHACHA WAMBURA, MAISHA, MWAIPOPO, HADUBINI, DAIRY YANGU na blogu zinginezo nyingi.

emu-three said...

Tuwenii macho na vitu kama hivi, sidhani kuwa tulianzisha blog zetu ili tupate hizo zawadi.
Ok, labda ni tuzo, na kama ni tuzo, hawo waandaji wapo wapi, na ni akina nani, na masharti au vigezoo vya hizoo tuzo ni vipi
Tuelewe kuwa nyanja hii ya mawasiliano imegubikwa na sintofahamu nyingi, wapo ambao kila kukicha wanabuni mbinu za kupata kwa kutumia migongo ya watu.
Hatuna uhakika na hili, kama lipo na watu wana nia njema, waweke wazi, sio mbaya mkawajali wanablog...cha msingi mjue kuwa wengi wa wanablog ni wapiganaji kwa ajili ya manufaa ya jamii, sio kwa ajili ya biashara au zawadi, kama zipo tutashukuru, sio mbaya.

Chib said...

Nilikuwa nimetingwa na kazi, kiasi kwamba suala hili la awards nilikuwa nasoma kicha cha habari lakini siingi kwa ndani, kwa sasa ndio nimepata picha baada ya kupitia blogu ya Kamala, Bwaya,Mcharia na hapa, na pia baada ya kusoma maoni ya akina Matiya, emuthree, Mtktf na wengine wengi. Nina mengi ya kujiuliza