Wednesday, May 18, 2011

Chemsha bongo...Mjini ni wapi?

Juzi kwenye ukurasa wa Facebook wa mdogo wangu nilikutana na maelezo yasemayo "While individuals embrace each other in rural, they stay apart in Urban."
Kisha nikawaza kuwa MJINI NI WAPI? Nikaweka majibu kuwa "Hivi Mjini ni wapi? Nikiwa Nyakibale niliona Omuluhamila kama mjini. Kufika pale nikaona Kaagya kama mjini, Na Kaagya wanaona Kashozi kama mjini na wa Kashozi wanaona Bukoba Mjini ndio kumekucha. Aliye Bikoba mjini anaamini Mwanza ndio kwen...yewe (tena anywhere in Mwanza) na aliye Mwanza anaamini Arusha ama Dar ama etc ndio haswaaaaa. Aliye Dar Kibondemaji anaamini Kariako ndio mjini na wa Kariakoo anaangalia Masaki. Wa Masaki anatazama Nairobi na nje ya nchi hata Marekani na hata hapa Marekani kuna aliye DC ama Los Angeles na bado anautafuta mji. KWANI MJINI NI WAPI? Labda hata ndani a nyumba yenu kuna mjini ambapo ni Master bedroom na aliye humo naye anaamini choo cha humo ndimo mjini mwake. KWA MAANA NYINGINE, LABDA MJI NA KIJIJI NI FIKRA TU. Kwa kuwa anayekula raha sana duniani na kuamini ana kila kitu, anaambiw na kuwa KUNA MBINGUNI KULIKO NA MANONO KULIKO ANAYOPATA. Labda huko ndio MJINI. Lakini tukifia huko hatutaambiwa kuna "mji mwingine?" NAWAZA KWA SAUTI TUUUUUUU..."
Na bado nawaza..........MJINI NI WAPI?

4 comments:

emu-three said...

Mkuu umetoa wazo la changamoto kweli, lakini mjini ni sehemu iliyojengeka vyema, ili inazidiana kati ya moja na nyingine.
Kwa msemo tukimaanisha `mjini' ni sehemu iliyoboreshwa zaidi ambapo huenda kuna kila kitu moyo unapenda, sasa wapi na vipi, hiyo inategemeana na mtu mwenyewe na nafsi yake!,

Yasinta Ngonyani said...

Mjini ni wapi? ,,,,je kama ni swali ndio hili mimi ningependa labda tungeanzia na wapi ni kijijini?...Nimekumbuka kitu nilipokuwa nyumbani Songea -Ruhuwiko kakangu akaniambia kuwa anaenda mjini nami sikumwelewa kabisa nikamuuliza mji gani akasema Songea mjini....kaaazi kwelikweli!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mhh shana. ila sasa kwa mlolongo wako, basi mjini ni marekani na ndio maana uko huko mpaka leo

Anonymous said...

mjini kwa kila mtu ni pale penye vitu ambavyo hajawahi kuvitumia ila havina uasilia. Ni pale watu wanapopishana bila kusalimiana wala kuulizana wamekula nini jana. Mjini ni pale huulizwi umevaa nini wala jina lako nani au unatokea wapi. Mjini ni pale unaweza kupata mpenzi bila kuulizwa imekuwaje? Mjini ni pale unapolala njaa hakuna anayeshangaa wala kujua ni vipi. Mjini ni pale unaweza kukopa bila kutangazwa kwa majirani. Mjini shule, mjini jalala la kila taka, mjini ni maendeleo ya kurudi nyuma na mbele maana utu hakuna, mjini hakuna wazazi ila baba fulani basi. Mjini bwana, we acha tu! hata aliye marekani kuna sehemu anapaita mjini. Anayekaa Pelham, Westchester count, anasema Manhattan ni mjini. Akifika pale Grand Central anataka aende Times Squre ndo aseme kafika mjini lakini wewe ukitoka Bugandika ukafika Pelham utafikiri umefika Dar! We acha tu!