Friday, May 20, 2011

Them, I & Them......NEVER GIVE UP....Luciano

Luciano kwenye onesho lake Zanzibar On The Waterfront 2008 Them, I & Them nayo ilikuwepo kudaka hili na lile"Many of life's failures are people who did not realize how close they were to success when they gave up." Thomas A. Edison (1847 - 1931)Nukuu hii ina ukweli mwingi na wa maana maishani mwetu hivi sasa. Wapo wengi ambao kutokana na mfumo wa maisha ulivyo na mkanganyiko wa uchumi wa sasa wameamua kuachana na kile wanachoamini na kukipenda na kujikuta wanajipotezea nafasi za kusonga mbele katika kukamilisha "mafanikio" yao maishani.
Pia nukuu hiyo hapo juu yanikumbusha kile alichokiimba hayati Lucky Dube katika wimbo wake TOUCH YOUR DREAM alipouliza "have you ever see the dream walking?, have you ever hear the dream talking? ....You are THE MASTER of your dream, if you pull the right string it'll be talking to you, don't hesitate, grab the chance before it's too late .... REACH OUT AND TOUCH YOUR DREAM"Tunalokumbushwa hapa ni kuwa maisha yetu yako mikononi mwetu. Tunaweza kuamua kufanyia kazi kile kilichopo mawazoni mwetu (ambacho wengine wanakiita NDOTO) na kisha kukifanya kuwa kweli (na hapo watakibatiza jina la UFUNUO).
Ama twaweza kubaki na "kumbukumbu" ya tulichokiota na kushindwa kusonga mbele.
Lakini maisha yetu hayajaumbwa kuwa marahisi na ndivyo ilivyo na inavyotakiwa iwe. Kwa maana nyingine, kupambana na majaribu ni sehemu ya maisha tuliyopangiwa.
Ni katika hili, tunakutana na Jephter Washington McClymont ambaye anafahamika zaidi kama LUCIANO, anapotueleza kuwa MAISHA YAMEPANGWA NA MUNGU na kupanda na kushuka ni sehemu ya maisha.
Ukisikiliza ubeti wa kwanza, Luciano anazungumzia wakati ambao maisha hutuendea vema nasi tukadhani ni haki yetu kuwa hivyo nasi kusahau kuwa MUNGU ndiye chanzo cha mtiririko wa maisha yetu na ni wajibu wa kila mmoja kulitambua hilo.
Anasema "Just like a river moving water on and on to the sea. Like an Ocean always in motion, that is how you got to be. Just like the wind that blows on a constant flow that gives us life wherever we go. Like the sun that shines and allows our days to go.. JAH IS THE SOURCE AND EVERYONE SHOULD KNOW."
Na katika kiitikio, Luciano anaendelea kutusisitiza kuwa licha ya ugumu wote huo, twatakiwa kuendelea kupigania kile tuaminicho mioyoni mwetu akisema "you should never give up, NEVER GIVE UP. Just keep on tyring. Never give up, believe in what you're doing. You should never give up, never give up. Have faith in what you believe in. ALWAYS BE FIRM WITHIN"
Lakini pia Luciano anaelezea wakati ambao mambo huwa yanakwenda kombo na baadae kuja kunyooka akituasa kuwa huo "ndio mfumo wa maisha" ambao MUNGU ameupanga na kwa kuwa yeye ndiye chanzo cha yoe, "hatutakiwi kushangaa".
Anasema "sometimes the crops refuses to bear and the harvest isn't really there. No rain the soil is cracked and dry, mothernature seems to die. Then one day shower came and the earth smiled again...... DON'T BE SUPRISED, 'CAUSE THAT'S NATURAL FLOW. JAH IS THE SOURCE AND EVERYONE SHOULD KNOW"
Na kwa wale ndugu zangu wote walio katika magumu ya uchumi, maradhi, ukiwa, kuuguliwa, ama harakati nyingine zionekanazo kukwamisha kile ambacho umekuwa ukipanga kufanya kwa muda mrefu, nakwambia alivyosema Luciano kuwa "You should never give up, never give up. Have faith in what you believe in. ALWAYS BE FIRM WITHIN"
Msikilize HAPA katika wimbo wake huo NEVER GIVE UP uliopo kwenye albamu yake ya Jah Is Navigator
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

No comments: