Sunday, June 19, 2011

Ikaribishe TONE INTERNET RADIO


Tunapenda kulitambulisha watanzania wote waishio popote Duniani kwamba kuanzia sasa wanaweza sikiliza Radio kupitia mtandao yani Internet Buree. Tumeona tufanye hivi kwa kutambua kwamba pamoja na kuwa watanzania wengi wapo hapa nchini na wengi wao kwa sasa wanatumia mtandao na wanapenda sikiliza Radio kupitia mtandao, lakini pia tumezingatia na watanzania wenzetu wanaoishi nje ya nchi wapate Burudani, Habari na mambo mengine mengi kutoka Tanzania. Kupitia Tone Internet Radio watakuwa hawajisikii upweke na kuona kama wapo Tanzania. Pia Tone Radio inawapa wasanii wa Muziki wa aina yoyote Tanzania kuleta nyimbo zao hapa studio na sisi kutangaza kazi zao bure kwa kututumia nyimbo zao kupitia toneinternetradio@yahoo.com . Karibuni sana nyote na pia ukisikiliza Radio mwalike na mwenzako. Pia tunapatikana katika Facebook profile yetu Tanzania Online-Radio

Tunatanguliza Shukurani Zetu za Dhati na karibuni sana... Tone Internet Radio Pamoja Tutafika

LINK: http://www.toneinternetradio.blogspot.com
Sillah Mbuya

No comments: