"Love can make so Happy,
Love can make you so sad,
love can make you so lonely,
Love can make you accomplish,
Love can make you go places,
Love can make you so strong,
Love can make you your future,
love can make you REMEMBER THE GOOD TIMES AND BAD TIMES, ....."
Spear aliimba mengi katika ukweli wa maisha ya mahusiano miaka ya sasa, lakini pia yalikuwa hivyo tangua zamani na bila shaka yataendelea kuwa hivyo.Mapenzi ni kitu kizuri saana kama kilivyo kibaya. Namaanisha uwezo wa uzuri wake ni sawa na uwezo wa ubaya wake iwapo yatakwenda visivyo ama kinyume na matarajio.
Katika kujikumbusha muziki wa kale, leo tunao wana Msondo Ngoma enzi hizo wakijulikana kama Juwata Jazz Band wakiwa naye marehemu Nico Zengekala ambao wanakuja na kibao chao SOLEMBA. Kisa mwanana juu ya binti aliyeamua kutotekeleza ahadi yake kwa mtindo / style ya kukomoa ambapo mwimbaji anasema alipomuuliza Solemba aliambiwa kuwa anajipendekeza kwake na yeye hampendi. Kama kuna kitu nilitamani, basi ni kusikia upande wa hadithi hii ukisimuliwa na Solemba mwenyewe kujua kama alichoimba Zengekala ndio hadithi kamili ama la. Labda itatokea, lakini kwa leo burudika na sehemu hii ya kisa SOLEMBA kama kisimuliwavyo naye Nico Zengekala
** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**
1 comment:
Oooh, Marehemu Nico Zengekala, kuna jamaa yangu mmoja alikuwa akipenda sana kuimba nyimbo zake, wakati tupo UMBWE...safi sana mkuu umenikumbusha mbali...TUPO PAMOJA!
Post a Comment