Sunday, July 10, 2011

Milionea...... bado anakusanya taka....ANAWAZA NINI?

Photo Credits: Dailymail.co.uk
UKISHINDA MILIONI KADHAA (tena namaanisha dola milioni kadhaa) UTABADILI VIPI MAISHA YAKO?
Nakumbuka mwaka 2000 nilikuwa nikiongea na Kaka yangu Lwaga Anangisye na katika maongezi akazungumza suala la NDOTO. Yeye aliliweka kwenye "lugha ya msisitizo" aliposema DREAMS. Kisha akasema neno ambalo mpaka leo likingali akilini mwangu. Kwamba "watu wengi wanaishia kutofanikiwa hata wanapopata nafasi kwa kuwa wanakuwa hawajajiandaa." Akasema kuwa wengi wetu hatuangalii lolote lililo zaidi ya uwezo wa sasa. Kisha akaniuliza, "ukipewa milioni moja sasa hivi ufanyie jambo la maana, utafanya nini?" Hilo pekee lilikuwa SWALI TOSHA KUNIAMSHA.
Nimekumbuka hilo baada ya kusoma kuhusu Bw Tyrone Curry. Mwanaume ambaye alishinda dola milioni 3.4 lakini bado anaendelea na kazi yake ya kusafisha vyoo na kukusanya takataka
Mzoa taka huyu ambaye aliwahi kuwa mwalimu, sasa ana kazi ya pili shuleni hapo ambayo ni kocha. Na kati ya zawadi alizotoa kwa shule "anayoitumikia" ni kuinunulia timu yake gari jipya lenye thamani ya dola 40,00.
Suala hapa ni kwamba licha ya kushinda dola milioni 3 na zaidi, Tyrone alipoulizwa kwanini anaendelea kufanya kazi anasema "You need to be doing stuff: That’s my philosophy.” Anapoulizwa kwanini anaendelea kuishi katika nyumba ya awali na hajabadilika, anasema "My mom was the mother of the neighborhood. All the kids came to our house, so that’s why my home is open, too. People come, they eat, and they have fun. Before I won the money, I struggled. Sometimes I fell behind, but I always remember my mom’s words: ‘You can have somethin’, but that person next to you might not have anything. If you look out for that someone, they’ll look out for you.’" na kisha kuhusu maisha yao (kama familia) anasema hayabadilika na "We don't even go out to dinner. We cook at home.”
Na ndio maana nikaanza kwa swali nililoanza nalo. ALIWAZA / ANAWAZA NINI KUFANYA KAZI LICHA YA UTAJIRI ALIONAO?
Tazama video inayomhusu hapa chini.***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya. Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***

2 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

lazima tuwe na vitu vya kufia, lazima tufanye baadhi ya vitu hata kama havitulipi, hasa upendo na kugawana kidogo tulicho nacho, AMN

Anonymous said...

na kama kwetu twajiita wasomi hata kufuta ubao hatuwezi. twpenda sana kuridhika bila ya kuwa na cha kuturidhisha.