Thursday, July 7, 2011

Si tatizo iwapo utaliangalia toka "pembe nyingine"

Wengi wenu mmeshuhudia UKIMYA niliokuwa nao mtanmdaoni. Tatizo kubwa lilikuwa ni MTANDAO. Na kwa juma zima nikahangaika na "provider" wangu kuweza kunirekebishia tatizo bila mafanikio.
Alipofanikiwa kurekebisha tatizo, akasema "kutokana na siku ambazo hukuwa na huduma, hatutakulipisha gharama kwa wiki nzima. Hivyo ankara yako ijayo itapunguzwa dola 21".
Fikra za awali zilikuwa ni kughafilika kwani niliwaza huyu "huyu mtu hajui ni kiasi gani nimeshindwa kuwasiliana na watu wangu, na anadhani thamani yake ni dola 21?"
Lakini muda mfupi baadae nikaliangalia "tatizo" toka pembe tofauti na nikagundua kuwa wamegawanya ankara yangu ya mwezi kwa siku nilizokaa bila huduma wakapata gharama hiyo, hivyo ndio gharama halisi.
Na badala ya KUKASIRIKA KUWA WANANIREJESHEA DOLA 21, ni vema nikafarijika kuwa NINALIPA DOLA 21 KWA JUMA ZIMA.

NILILOJIFUNZA ni kuwa badala ya kukasirika kuwa nimepunguziwa kiasi kidogo cha dola 21, ninaweza kumshukuru Mungu kuwa gharama ya mawasiliano ya simu na internet kwa siku zote nilizokosa ni dola 21. Hii ilinifanya nione kuwa si tatizo. Sio kwa sababu lilitatuliwa, bali kwa kuwa nililiangalia kutoka PEMBE NYINGINE. Na hilo limenifanya nitambue kuwa katika mengi tuonayo, yawezekana SI TATIZO IWAPO TUTAYAANGALIA TOKA "PEMBE NYINGINE"

3 comments:

Simon Kitururu said...

Mmmmh!

Fadhy Mtanga said...

mmhhhhh! Kama Mtakatifu Simyoni

Unknown said...

Ooooh POLE. Nayo ni changamoto.