Sunday, July 31, 2011

RAMADHAN NJEMA NDUGU ZETU

Kwa siku kadhaa zilizopita, asilimia kubwa ya takribani watu Bilioni moja waumini wa dini ya Islamu wamekuwa wakijiandaa kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa tisa na MTUKUFU zaidi katika kalenda ya kiIslamu.
Mwezi huu uambatanao na mafunzo na njia sahihi za kuishi kiIMANI, na uwe nguzo ya maisha yetu hata baada ya kumalizika kwa mwezi huu
Yafunzwayo na kuhimizwa kwenye mfungo na mwezi mzima, ni mambo ambayo naweza kuyaita NJIA SAHIHI ZA KUISHI KATIKA JAMII na ninaamini yale yafunzwayo na maisha tuishiyo mwezi huu, tutayaendeleza maishani
Blogu ya CHANGAMOTO YETU yawatakia wale wote wafungao na kuamini katika mwezi huu, MWEZI NA MFUNGO MWEMA na kwa wale wote waishio na waamini twawatakia ushirikiano mwema kwa waamini
RAMADHAN KAREEM.

5 comments:

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Bwana Bandio nimesoma kwenye blog ya CCM ya Michuzi kuwa ulikuwa na mahojiano na fisadi wa EPA Mwanaidi Maajar. Mbona huyachapishi?
Nayaongoja kwa hamu kusikia mikakati yake hasa kuhusiana na NGO ya mumewe ya kutafutia ulaji na kibarua ili asionekane kula kulala.

Mzee wa Changamoto said...

Heshima kwako Mwalimu.
Kwa hakika nilikuwa kwenye mkutano naye kama ulivyoona kwenye hiyo blog ya Michuzi. Lakini hayakuwa mahojiano haswa, ilikuwa ni katika kueleza mikakati ya Ubalozi katika kuwashirikisha waTanzania katika kusherehekea miaka 50 ya Uhuru hapa U.S.A
Kwa hiyo hatukuwa na "maswali na majibu". Na pia sijawa familiar sana na suala la EPA. Niliona kwenye "cut out" ya picha ya gazeti kwenye mtandao mmoja, lakini sijabahatika kuwa na details. Kama unazo ama ulishaandika nika-miss ama hata kama ziliandikwa mahala pengine naomba unisaidie link ili nipatapo muda wa mahojiano nimuulize atueleze, kwani naamini ataeleza kwa kuwa amekuwa akisema yeye ni muwazi.
Baraka kwako Mwalimu

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kaka nimekupata. Kujua anachojua kuhusiana na ufisadi wa Richmond au EPA, just muulize ajuacho kuhusiana na kuhusishwa kwa kampuni yake ya uwakili ya REX. Very simple.

SERENGETI GRILL said...

shukran

emu-three said...

Mkuu ujumbe mwema kabisa, na wewe pia TWAKUTAKIA RAMADHANI NJEMA,....TUPO PAMOJA