Sijui ni kwanini tunaiga mengi lakini hatupendi kuiga mengi-ne ambayo yaendana na mengi hayo? Yaani "tunaigilishwa" Demokrasia lakini bado tunaambiwa ndani mwake kuna "yasiyoendana na mila na tamaduni zetu". Na hapo ndipo ninapokuja kuwaza KWANINI TUIGE BASI?
Jana nimesoma (kupitia mitandao) kuwa mchakato wa kampeni jimbo la IGUNGA unaelekea kushika kasi. Nikakumbuka lileee suala la matangazo ya uzinduzi wa kampeni za CHAma cha DEmokrasia na MAendeleo (CHADEMA) kukatishwa na kituo cha televisheni ya Taifa (TBC1) kwa kile kisemekanacho kuwa mkutano huo ulianza kuzungumzia watu binafsi.
Hizi zilikuwa habari za kusikitisha lakini si za kushangaza hata kidogo kwa nchi yetu.
Upashanaji habari kwa waTanzania wala si jambo la HAKI, bali UTASHI. Na niliwahi kuuliza TAARIFA.......HAKI YA WANANCHI AMA? (irejee hapa).
Lakini tuachane na upashanaji habari pekee. TUANGALIE VIONGOZI WETU
Unakumbuka alichoandika Da Subi kuhusu hotuba za Mwl Nyerere?(hapa). Yaani baadhi ya watu wanazuia hata HOTUBA ZA Mwl NYERERE (zirejee hapa) kusikika ama kuchapishwa ati kwa kuwa hawana HAKIMILIKI.
Ni kweli kuwa tatizo ni hakimiliki? Ama kwa kuwa ZITAWAZINDUA WANANCHI KUHUSU LIENDEALO DUNIANI?
Hivi majuzi nimemsoma Kaka Ngurumo namna alivyotishwa na serikali juu ya maswali yake magumu (rejea hapa) kisha nikawaza, kama Rais akiulizwa maswali haya anakuwa mkali, ingekuwaje kwa Pink aliyemuomba Rais Bush "kutembea naye na kumuuliza" haya hapa chini?
Ama angefanywa nini msanii yeyote kama angeamua kuunga hotuba za Rais na pichaze kama alivyofanya binti huyu hapa chini?
Labda ufike wakati watu wapewe haki ya kusema kile waaminicho kuwa sahihi kisha mahakama iwajibike kuwahoji na kuwataka wathibitishe wasemacho na si vyombo kama Maelezo na TBC kuwa wahukumu wa kisemwacho juu ya viongozu na hata umiliki wa hotuba hizi za viongozi muhimu kama Baba wa Taifa.
***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment