Sunday, August 7, 2011

Harambee kuchangisha pesa za kusafirisha mwili wa Marehemu Macrina kufanyika tena leo jumapili.

Leo, Jumapili Aug 7,2011 Saa 9 alasili (3pm), harambee ya kukusanya pesa kwa ajili ya kusafirisha mwili wa Marehemu Macrina Samaka (pichani juu) itaendelea nyumbani kwa Bwn Arthur Gao (anwani imewekwa chini).

Harambee iliyofanyika Jumamosi ya Aug 6,2011 iliwezesha kupatikana kwa kiasi cha $2,532/=. Kwa kiasi hiki, bado kiasi cha $ 6468 kinahitajika kuweza kufikisha $9000 zilizokadiriwa kama gharama za kurudisha mwili wa marehemu Macrina Samaka nyumbani Tanzania.

Harambee hizi huendeshwa kwa mnada wa kile kiletwacho (kama khanga) na fedha yote kuongezwa katika mfuko unaotunishwa kuwezesha usafirishaji wa mwili wa Dada Macrina. Hivyo tunaomba kila mwenye uwezo wa kuchangia ama kutoa kitakachoweza kunadishwa, kufanya hivyo ili kuwezesha hili.

Address ya msiba ni
4303 FRANKFORT DR,
ROCKVILLE,MD,20853

Pia tunaomba viongozi wa Jumuiya za waTanzania katika majimbo mengine kuwafahamisha wanachama wao ili walio na uwezo wasaidie kukusanya michango. Kwa wale mbali na hapa, na ambao wangependa kuwasilisha michango yao (ambayo kwa hakika inahitajika), wanaweza kuiweka kwenye akaunti maalum iliyofunguliwa maalum kuwezesha ukusanyaji michango huu. Routing #055003201-A/C #1010323780193-WACHOVIA BANK-Arthur Gao/Memorial Funds a/c for Macrina Samaka.

kwa mawasiliano zaidi na maelekezo ya ziada waweza kuwasiliana na yeyote kati ya hawa

Afisa Ubalozi,Abass Misana-202 378 8066
Rasheed Mkakile-240 938 3177
Arthur Gao-240 408 1422
Magrette Wahida-301 915 5821
Dj Luke Joe-301 661 6696
Malecela(New York)-914 473 1033
Boston(MA)
Juliana-413 330 3891
Abela- 781 913 2107Suzie-617 306 1645
Houston,TX
Georges Assenga-713 894 9403
Wichita,KS
Erick Tagalile
316 993 0843Bruce Bond-301 254 2806

MWENYEZI MUNGU AMETOA,MWENYEZI MUNGU AMETWAA NA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
AMIN

No comments: