International Women's Day

International Women's Day

IMETOSHA

IMETOSHA

KUMRADHI

Kutokana na kubanwa na masomo, mabandiko hayatakuwa kila siku kama awali.
NAWAPENDAWednesday, August 10, 2011

"Nami si mimi". Wapongeze ama kuwalaumu hawa.....

Na wewe pia......
Ni siku mpya maishani mwangu. Siku inayoashiria kuanza kwa mwaka mpya. Mwaka unaoanzisha mzunguko mpya (na naamini) mwema maishani mwangu. Wengine wanaita SIKU YA KUZALIWA. Lakini kama nilivyowahi kusema ( hapa na hapa), maisha yamekuwa zaidi ya shule. Na ni shule hii inayoniumba na kunibumba. Inani-shape kwa namna moja ama nyingine. Kuna wale wanizungukao, niwasikilizao na kufanya wafanyayo, na ndio wanaonifanya niwe mimi na si vingine, na pia wale ambao sipati nafasi ya kuwa kama ambavyo wangeweza kunibadili ama kuathiri maisha yangu. Na hii ndio dunia niishiyo. Labda ningekuwa mwema, lakini LABDA ningekuwa hovyo. Ila niko nilivyo na licha ya kuendelea kuboresha u-mimi wangu, bado naupenda na kuuheshimu (huo u-mimi).
Mbali ya WAZAZI NA NDUGU (wa lazima na hiari) ambao kila mara nawatolea shukrani kwa uwepo wao kwangu, nimejifunza mengi kutoka kwa marafiki, na hata wale wanaojiona kama maadui kwangu. Nyote mmenifunza, na nyote mmenikuza. Nimekuwa mimi sababu ya changamoto mnazonipa na natumai kuwa nyingine nyingi zaja. Nashukuru kwa UMOJA uliopo (ule chanya na hasi) na
Kwa Baba na Mama, Baba na Mama wakubwa na wadogo, Wajomba na Mashangazi, Mabinamu, Kaka na Dada zangu (wote wakubwa na wadogo), ndugu wote wa hiari na marafiki mnaonifanya NIKUE, nawapenda sana.
Nililojifunza maishani ni kuwa KILA MTU ANA FUNZO, KILA MTU NI SHULE NA KILA MTU NI MUHIMU. Hata kama shule hiyo ni kukufunza usichotakiwa kufanya.
Nawapenda sana, nawathamini na nawaheshimu mno. Ninyi kwangu ni sehemu kubwa ya mimi, na SIFA na LAWAMA zote zije kwenu.
NIWE MUWAZI NA MKWELI. Maisha ya sasa yasingekuwa yalivyo bila msaada mkubwa wa wapendwa wangu wakuu wawili. Mke wangu Mpenzi Esther na mwanangu Paulina.
NAWAPENDA na NAWAHESHIMU mno. Nina kila sababu ya kujivunia kuwa nanyi.
Nakumbuka na kurejea taswira za awali maishani

12 comments:

Albert Kissima said...

Kaka hongera kwa mwaka mwingine mpya. Ninafurahia na ninazidi kujivunia uwepo wako. Mungu akutunuku miaka mipya mingi yenye furaha na Mafanikio tele kwa kadiri ya upendavyo.

Mzee wa Changamoto said...

Asante sana ndugu yangu.
Naheshimu sana uwepo wako.
Baraka kwako

kijah said...

Hongera kwa kuzaliwa upya my kaka!!! mungu awakupe maisha marefu zaidi yenye furaha na amani, wewe na familia yako..

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana kwa siku yako ya kuzaliwa. Ni jambo la kufurahi sana siku kama hii inapokuja maana unakuwa unazaliwa upya tena na namba zinaongezeka...:-) Wabarikiwe wazazi na wengine wote waliokuwa karibu nawe. Kuwa wewe kama wewe ni faida kwa sisi wengine. UWE NA SIKU NJEMA.

Fadhy Mtanga said...

kaka nilitamani sana kuweka bandiko la kukupongeza pale kibarazani kwangu. lakini nipo Mbeya na network naipata kwa kuvizia sana.
nimefurahi nimekuja kupata mahali pa kukutakia siku njema ya kuzaliwa.

wewe ni mmoja wa wale wanablog ambao najivunia sana kuwafahamu.

kaka, ningeweza kusema mengi saaaaaaana. lakini yote ambayo ningeweza kuyasema yanaweza tu kuwakilishwa na sentensi moja.

HERI YA SIKU YA KUZALIWA KAKA MUBELWA, UWE NA MAISHA MAREFU SANA.

EDNA said...

Hongera sana kaka, Mungu na akupe miaka mingi zaidi duniani na akutimizie yale utamanio moyoni mwako.

Ebou's said...

Tunamshukuru sana M/Mungu kwa kutujalia uzima na afya jeema katika siku hii leo. Pia tumshukuru kwa siku hii muhimu sana kwako Mzee wakuvumbua Mubelwa Bandio, kwa siku hii adhimu ya kuzalia kwako, wadau wote wa swahilivilla wanakutakia siku njeema, maisha marefu ya kujitanafasi, wewe pamoja na familia yako inshaallah. ''Ameen'' HAPPY BIRTHDAY TO YOU http://swahilivilla.blogspot.com/2011/08/kheri-ya-kuzaliwa-kwako-mubelwa-bandio.html

Mija Shija Sayi said...

Hongera sana kwa siku yako ya kuzaliwa kaka, ninakuombea kila la heri katika maisha yako...Mungu akulinde pamoja na familia yako.

God bless!!

SIMON KITURURU said...

Hepi siku MPYA mkuu! Ila tatizo ni kwamba jana ni kama leo tu usipodeku kimakini!:-(

emu-three said...

HAPPY BIRTHDAY MKUU. MUNGU AKUJAZE BARAKA, AFYA NA FURAHA AMANI NA MAFANIKIO TELE...AMINI

PASSION4FASHION.TZ said...

Hongera sana kaka kwa siku yako ya kuzaliwa,mungu azidi kukupa afya njema,na akuongezee hekima.
furahiya siku yako kaka.

Nimeipenda sana hiyo picha ya familia yako hapo chini.

Subi said...

Heko kwa kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa.
Uendelee kupata baraka nyingi na afya njema katika maisha yako na familia yako!