Saturday, September 24, 2011

Da Mina apumzishwa

Maisha ya Dada yetu Mina Said Omar hapa duniani yaitimilika Septemba 21 hapa Maryland. Maisha mapya yameanza. Na kati ya maisha ya kale na mapya, kuna hatua za kupumzisha mwili. Na ndilo lililofanyika jana katika makaburi ya Al firdaus Memorial Gardens yaliyopo bara bara ya New Design, Frederick, Maryland nchini Marekani.
Baadhi ya wapendwa waliweza kutuwakilisha katika tukio hilo na TUNAWATHAMINI KWA HILO. Kaka yetu Ebou Sharty wa blogu hii ya Swahili Villa alihudhuria na kuweza kushirikiana nasi baadhi ya kumbukumbu
Jeneza la Marehemu Mina Said Omari likipelekwa ndani ya msikiti wa Islamic Society uliopo Frederick, Maryland.
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Mina Said Omari, aliyefariki siku ya Jumatano Sept 21, 2011 saa 4 usiku (10pm) Frederick Memorial Hospital likiwa ndani ya msikiti wa Islamic Society uliopo Frederick, Maryland kwa ajili ya kusaliwa.
Ndugu jamaa na marafiki wakiwa ndani ya msikiti wa Islamic Society uliopo Frederick Maryland
Waumini wa kiIslamu wakijitayarisha kwaajili ya sala ya jeneza
Waumini wakitoka msikitini baada ya sala ya ijumaa pamoja na sala ya maiti tayari kuelekea makaburi ya Al firdaus Memorial Gardens yaliyopo bara bara ya New Design, Frederick, Maryland.

Kwa picha zaidi toka BLOGU YA SWAHILI VILLA, BOFYA HAPA
PUMZIKA KWA AMANI Da MINA