Friday, September 9, 2011

Equal Rights.....Peter Tosh

Siku mbili zijazo, Marekani (na sehemu nyingine za dunia) zitakuwa zikiadhimisha miaka 10 tangu kutokea kwa mashambulizi makubwa zaidi kufanyika katika ardhi ya Marekani katika miaka ya karibuni. Ni mashambulizi haya ambayo yamebadili ulimwengu hasa kwa upande wa USALAMA. Si jambo rahisi kutetea upande wowote unaoamini kuwa dunia imekuwa salama kabla ama baada ya mabadiliko yaliyotokana na shambulizi hili, lakini ukweli utabaki palepale kuwa CHANZO CHA VITA VINAVYOENDELEA HAUJATAFUTWA, HAUJAJULIKANA NA WALA HAUJAFANYIWA KAZI. Na hili ndilo linalosikitisha na kutisha. Sijui ulikuwa wapi, ulikuwa ukifanya nini ama nini kiliendelea, lakini siku hii iliyobadili maisha yetu itabaki kukumbukwa kwa namna nyingi na wengi. Nakumbuka nilikuwa nimetoka Mbagala kwa Baba Mdogo na nilipofika nyumbani Kurasini nikawasha Tv ili niangalie maendeleo ya michezo ya kimataifa kujua mabadiliko na nini na kipi cha kuwekea mkazo katika anga za kimataifa kwenye kipindi cha michezo jioni hiyo pale Times FM nilipokuwa nikifanya kazi. Nilipowasha Televisheni nikakutana na habari hii . Iliniumiza saana kuona watu wakiwa ghorofa zaidi ya mia wakishuhudia namna wasivyo na namna ya kuifikia ardhi wakiwa hai. Kwa wengi wa kizazi hiki, tukio hili la Sept 11 2001 laweza kuwa moja kati ya yale machache ambayo mpaka sasa tunashuhudia athari zake ulimwenguni kote. Ni tukio ambalo lilisikitisha saana kwani maisha ya wengi WASIO NA HATIA yalipotezwa.
Sitaki kuingia katika kusaka chanzo cha tukio hili, lakini hakuna ubishi kuwa kukosekana kwa HAKI NA USAWA KWA WOTE kumekuwa tatizo kubwa katika yale yaendeleayo sasa. Haijalishi nia ya watendaji ilikuwa nini, ila kushindwa kusaka walio kiini cha matatizo yao na kuua wasio na hatia ndio chanzo cha malipizo tunayoyaona yakiendelea sasa hivi. Marekani iliamua kwenda kuwasaka waliohusika na katika kusaka huko inaendelea kujikuta ikisababisha vifo kwa wasiohusika. Vifo hivyo vinazidi kujenga chuki na nia ya visasi na tunaona kuwa jinsi vita inavyoendelea ndivyo visasi vinavyoongezeka. Yaani ni kama tunaongeza akiba ya visasi baina yetu kwenye akaunti ya chuki tuliyojifungulia. Luciano aliimba akisema "we kill the wicked but still more rise, without proper justice we shouldn't be suprised." Ina maana kuwa waliosababisha haya yaliyotokea Sept 11 walikuwa wakilipiza kisasi kwa wanayoamini wanastahili lakini wakayatenda kwa watu wasio na hatia. Na hili ndilo tatizo la kutokuwa na HAKI NA USAWA.Leo hii, tunapoelekea kukumbuka miaka 10 hii ya shambulizi hili, tunaye Winston Hubert McIntosh ama Peter Tosh ambaye naye aliuliwa na aliyekuwa rafiki yake Dennis 'Leppo' Lobban tarehe kama hiyo hiyo lakini miaka 24 iliyopita ( Sept 11 1987) Tosh aliwahi kuimba kuhusu tatizo la haki na usawa katika wimbo wake wa EQUAL RIGHTS na alilieleza kama chanzo cha matatizo mengi makubwa kwa kuwa watu wengi hawataki kutafuta suluhisho la matatizo na kujikuta wanakwepa na "kuendeleza" tatizo. Mfano ni watu kujifanya wakitafuta amani huku wakipuuzia haki na usawa na wengine kutamani kwenda mbinguni lakini hawataki kufa. Mmmmmmmhhh!!!!!!
Msikilize huku ukisoma mashairi yake na kumtafakari

Everyone is crying out for peace yes
None is crying out for justice
(2x)

(CHORUS)
I don't want no peace
I need EQUAL RIGHTS AND JUSTICE (3x)
Got to get it
Equal rights and justice

Everybody want to go to heaven
But nobody want to die
Everybody want to go to up to heaven
But none o them (2x) want to die


CHORUS
(Just give me my share)

What is due to Caesar
You better give it on to Caesar
And what belong to I and I
You better (2x) give it up to I

CHORUS
(I'm fighting for it)

Everyone heading for the top
But tell me how far is it from the bottom
Nobody knows but
Everybody fighting to reach the top
How far is it from the bottom

CHORUS

Everyone is talking about crime
Tell me who are the criminals
I said everybody's talking about crime, crime
Tell me who, who are the criminals
I really don't see them

CHORUS

There be no crime
Equal rights and justice (Precedes each line below)
There be no criminals
Everyone is fighting for
Palestine is fighting for
Down in Angola
Down in Botswana
Down in Zimbabwe
Down in Rhodesia
Right here in Jamaica


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:

sophia said...

asante sana dah ubarikiwe daima hayo ndio mambo yangu ninayo yapenda sasa hapo umenikamata zaidi i love to read more kuhusu mambo kama hayo kaka

Simon Kitururu said...

Mmmmh!
Kipele chema kiukunaji MKUU!