Monday, September 12, 2011

Harambee nchini Uingereza kuchangia wahanga wa Zanzibar



Jumuiya ya waTanzania nchini Uingereza TANZ-UK ikishirikiana na Jumuiya ya Wanzanzibar waishio Uingereza (ZAWA), Urban Pulse na Miss Jestina George Blog imeandaa harambee (fundrising) maalum kwa ajili ya kuweza kuwasaidia waathirika wa ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea Nungwi njiani kuelekea Pemba. Fundrising hii itafanyika katika Ubalozi wetu hapa London tarehe 17 Septemba 2011 Kuanzia saa nane mchana.

Tunawaomba Watanzania wote mlioko hapa nchini Uingereza kutoka jumuiya mbalimbali,vyama vya kisiasa, wafanyabiashara, wanafunzi na hata wasio Watanzania mjitokeze kwa wingi ili kuweza kujumuika nasi na kufanikisha zoezi hili. Hivyo basi tunaomba mwenye fedha au chochote kile cha kuweza kuthamanishwa tunaomba tuweze kuja nacho na kitafanyiwa mnada. Mfano, wenye biashara wanaweza wakaleta bidhaa kiasi ambazo zitafanyiwa mnada ambapo ziada itakayopatikana itakuwa sehemu ya mfuko tutakaokuwa tunautafuta.

anwani ni; 3 Stratford Place, London, W1C 1AS. Muda ni saa nane mchana (2pm sharp).
Kwa maelezo zaidi tunaomba uwasiline na ...............
Mwenyekiti Tanz-UK 07766856565,
ZAWA 07538063536,
TA London 07404332910
UKIONA TANGAZO HILI TAFADHALI MTAARIFU NA MWENZAKO. WOTE TUNAKARIBISHWA, Mungu ibariki Zanzibar, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa . Zaidi sana Mungu wabariki Watanzania wote popote pale walipo duniani.

ASANTENI.
MWENYEKITI,
TANZ-UK

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Tupo pamoja..kwani ni msiba wa kila mtu ...Mwenyezi Mungu na atupe nguvu hasa waliofiwa kwa kipindi hiki kigumu.