Friday, September 16, 2011

Till you lose it all..............Lucky Dube

Libya, Libya, Libya.
Ni nani ambaye hajasikia habari zake hivi karibuni? Habari za UKOMBOZI na DEMOKRASIA. Kama unavyoona pichani, wapo wengi wanaoamini kuwa LIBYA itakuwa njema bila Gadaffi. Wanaweza kuwa sahihi, lakini ninaloonya ni MAISHA YA WATOTO wengi ambayo yameathirika sasa, na pengine kwa miaka yote ya maisha yao kutokana na maamuzi ya WACHACHE.
LIBYA.... Nani anayejua maisha waliyokuwa wanaishi kabla ya vurugu hizi? Nimesoma sehemu mbalimbali kuhusu maisha ya waLibya kabla ya vurugu hizi, na unawaza kama kulikuwa na ukweli. Tumesoma kuhusu
Mikopo kwa wananchi wa Libya ilitolewa bila riba.
Malipo kwa wanafunzi na wanaotafuta vyuo nje ya nchi.
Mafao kwa wanandoa.
Elimu na huduma za afya bure.
Elimu. Takriban robo ya wananchi wana elimu ya chuo kikuu.
Haya yote yanaonekana kufanyika kwa sababu nchi ilikuwa ina rasilimali ambazo ilizitumia kwa manufaa ya wananchi. Nimesoma habari za pesa alizonazo Gadaffi, na pia namna ambavyo amekuwa akiishi maisha aghali, lakini nauliza kuwa iwapo utaangalia uwiano wa maisha ya Gadaffi na wananchi wake, ukalinganisha na maisha ya viongozi wetu na wananchi wetu, ni nani mwenye kuwaibia wananchi zaidi?
Ninasikitisha kuona SHANGWE zinazoendelea baada ya kuonekana kuanguka kwa utawala wa Gadaffi, lakini naona watu wanapuuzia hali halisi ya maisha. Kuwa WANANCHI WA LIBYA SASA WANAKATA TAWI WALILOKALIA.
Wamepewa MSAADA WA MUDA MFUPI toka jumuiya mbalimbali lakini NINA HAKIKA kuwa punde baada ya kukamatwa, kufa, ama kuhakikishiwa kuwa Gadaffi hayupo nchini Libya, msaada utapungua na pengine kuisha. Na ni hapo ambapo ninaanza kuwa na wasiwasi wa namna ambavyo nchi itaweza kupata pesa za kujiendesha.
-Viwanda vilivyokuwa vikitoa ajira kwa maelfu ya watu baadhi vimeharibiwa,
-baadhi ya visima vya mafuta vilivyokuwa chanzo cha pesa na ajira kwa wengi
-barabara zimeharibika
NA KUBWA ZAIDI... WANAOCHUKUA MADARAKA HAWAAMINIKI. Hivi majuzi tumesoma wasiwasi wa kuwepo kwa Al-Qaeda miongoni mwa "waasi" na hilo linaanza kutishia mtitirisho wa pesa kwa waasi hao. Na pia miongoni mwa VIONGOZI AMA WAUNGA MKONO WAASI ni wale ambao kwa sehemu kubwa ya maisha walikuwa na Gadaffi na hawakuwahi kumpinga Mheshimiwa Rais. Je...Ni wanaMapinduzi halisi ama ni waroho ambao walikuwa chini ya MDHIBITI GADAFFI na sasa WAKO HURU KUIBA NA KUFANYA WATAKALO?
Pengine nia haswa ya kumtoa Gadaffi ilikuwa ni kuboresha maisha ya waLibya na kutumia pesa alizokuwa "akiingiza" Gadaffi kuboresha nchi ya Libya. Lakini ninalowaza ni kuwa NDOTO hii inaweza isitimie kwa kuwa vyanzo vya pato vimetenguliwa, na sasa tunasikia waasi wakiomba pesa za kuwawezesha kuendesha harakati zao na hili linanifanya niwaze kama watakuwa na uwezo wa kuongoza nchi.
Ninaloomba ni waLibya kufanikiwa, na si kuingia kwenye yale yaliyoikuta SOMALIA ambayo haijatengemaa tangu kuondoka kwa Siad Barre ambaye utawala wake uliangushwa na Mohamed Farah Aidid mwezi Januari mwaka 1991.
Na kwa kuwa ni Ijumaa, tumalize mazungumzo kwa kumsikiliza Lucky Dube na kibao chake TILL YOU LOSE IT ALL ambao unaonya juu ya kuthamini tulichonacho na si kusubiri kujilaumu. Libya wajifunze kutoka kwenye mifano kama hii ili wahakikishe kuwa hawajutii maamuzi wafanyayo.
Phillips Lucky Dube, na kibao TILL YOU LOSE IT ALL. Msikilize hapa huku ukifuatilia mashairi

We take a lot of things for granted, One day it' ll be taken away
That's when you'll realize how important it was
You never miss your water till your well runs dry
Give thanks and praise all the time
The wolf is always by the door

Chorus:
You don't know what you've got
Till you lose it all again
You never miss your water
Till your well runs dry

He's a hero, now that he' s dead
Oh what a bull, preacher man talks about him
When he was alive he didn't even know his name
When he was alive he didn't get this love
You never miss your water till your well runs dry

Chorus:
You don't know what you've got
Till you lose it again
You never lose your water
Till your well runs dry


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kwa ruhusa yako na hata bila ruhusa nitaitumia makala hii kama ilivyo kwenye mitandao jamii mingine niiandikaiyo, ni fundisho

ila umesahahau hta mfano wa IRAQ.

sera za wazungu ni za ajabu, waafrika hata hatujiulizi, tunaona wadhungu wanatupenda kama baba na mamazetu kiasi cha kutuondolea mbaya

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Kamala.
Wewe endelea tu na kusambaza ujumbe ndugu yangu.
Kuhusu IRAQ, kwenye aya ya pili toka mwisho kuna senteni inayosema "Libya wajifunze kutoka kwenye mifano kama hii ili wahakikishe kuwa hawajutii maamuzi wafanyayo. na hiyo ni link ya masuala ya Iraq, Afghanistan, Iran, Somalia na kadhalika.
Sikutaka kuirefusha sana na kwenda nje ya mada kidogo.
Shukrani kwa kuendeleza kuielewesha jamii
Baraka kwako Baba "Mjenzi".
TUIJENGE JAMII