Wednesday, September 7, 2011

Wawakilishi wa Tanzania katika Bunge La Vijana London

Kushoto Lucy na Linda katika picha ya pamoja Ubalozini
Ubalozi wetu wa Tanzania Hapa Nchini Uingereza Kwa Kushirikiana na Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania wamewateua Linda Kapinga na Lucy Minde ili kwenda kutuwakilisha katika mkutano wa nne wa Commonwealth Youth Parliament ( Bunge la Vijana) ulioanza tarehe 6-10 Septemba 2011 jijini London. Mkutano huu Umeandaliwa na Commonwealth Parliamentary Association tawi la Uingereza ikishirikishwa na Sekretarieti ya CPA ambayo ni Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola. Katibu wake ni Mwafrika wa kwanza kuteuliwa na Pia ni Mtanzania mwenzetu Dr William Shija.

Lengo kuu la mkutano huu ni kuwawezesha vijana kati ya miaka 19-29 kwa kuwapatia uzoefu wa shughuli za Bunge hasa katika kuimarisha demokrasia ya mabunge na Uchumi. Motto wa Mkutano wa mwaka huu "MABADILIKO YA HALI YA HEWA"

Ubalozi wa Tanzania hapa Uingereza unapenda kuwapongeza sana Linda Kapinga na Lucy Minde kwa kuchaguliwa kwao na pia kuwatakia kila la kheri katika kutuwakilisha kwenye mkutano huu.
Mh Naibu Balozi katika picha ya pamoja Lucy na Linda walioteuliwa kutuwakilisha katika Bunge la vijana
MH Naibu Balozi kwenye picha ya Pamoja akiwa na baadhi ya maofisa wa ubalozi, TMK na mapromota wao waliokuja kuwaunga mkono Linda na Lucy
Linda Kapinga, mteuliwa mmojawapo Urban Pulse na Miss Jestina wakifanya mahojiano na Linda Lucy Minde, mteuliwa wa pili
Lucy akitoa ufafanuzi wakati wa mahojiano


IMETOLEWA NA
Urban Pulse ikishirikiana Miss Jestina Blog Na Ubalozi wa Tanzania

No comments: