Friday, October 28, 2011

WHAT A DAY.....Tanya Stephens

"I'm tired of the hunger I see on people's faces. Tired of the animosity between the races. Tired of corruption in high and low places and pricks with money but no social graces..".
Ndivyo aanzavyo mwadada Tanya Stephens. Mmoja kati ya "vichwa" halisi vya muziki wa reggae kwa sasa na ambaye ameonekana kuwa na msimamo mkali kwenye mambo mengi aiimbiayo jamii yake. Ni kweli nami nimechoshwa na NJAA iliyokithiri kiasi cha kujionesha kwenye nyuso za watu, nimechoshwa na RUSHWA iliyo ngazi zote na hata TAKWIMU nzuri za ukusanyaji kodi na mapato lakini HAKUNA NEEMA KWA JAMII YA CHINI. Lakini kama kuna mstari ambao Tanya kanifanya nijiulize mara nyingi ni ule asemao "am tired life and death being sold as a pair..." na hapo najiuliza maswali mengi kuhusiana na maisha na jamii yetu ya sasa.

Je! alikuwa akiwazungumzia madaktari ambao huwasaidia watoto kutoka tumboni mwa mama zao salama lakini wakati mwingine kusaidia utoaji mimba?

Je! Anafikiria jinsi binadamu tunavyojitahidi kusaidia kuendeleza maisha kwa kuhimiza uzinzi (matumizi ya kondomu badala ya elimu m'badala juu ya Ukimwi)

Je! alikuwa akizungumzia majaribio ya tiba zitakazosaidia kuokoa maisha na ambayo wakati mwingine yanaleta maradhi yasiyotibika?

Je! alikuwa akiwafikiria wanaopenda mafanikio ya wananchi wao na kugombea uongozi kisha kuanzisha vita vinavyoua wananchi hao wasio na hatia?

Je! Alikuwa akizungumzia nchi zinazohimiza amani kwa kuua "waasi"?

Je! anazungumzia nchi ambazo zinazalisha vyakula na silaha kwa wingi kisha kuchonganisha mataifa yaongozwayo na "wavivu wa fikra" na vita ikianza wanawauzia chakula waishi na silaha waendelee kuuana? Kuna maswali mengi ila Tanya anaendelea kwa kusema amechoshwa na "politicians who keep say they care..." Lakini anaendelea (kwenye bridge) kueleza kuwa yawezekana mabadiliko ni ndoto, na yawezekana maisha si mabaya kama tuonavyo, lakini kwake yeye kama njia pekee na bora kufanya ni kuota, basi ataendeleza ndoto maisha yake yote. Kubwa ni sehemu iliyobeba jina la wimbo na maana halisi ya maisha ya sasa na hasa Barani Afrika akisema itakuwa siku ya furaha saana siku ambayo vita itakuwa kitu cha kupita, na amani kuwa ya kudumu. Siku ambayo thamani halisi ya maisha itajulikana na siku ambayo watu wataishi sawa na vile wahubirivyo. Siku ambayo UPENDO hautakuwa nadharia tu na damu kuacha kutiririka mitaani. Anasema "What a day when war becomes a thing of the past and peace we will have it at last and life is finally worth its cost and oh oh oh.
What a day when men finally live what they teach and
love aint just a concept we preach and blood no longer runs in the streets.."
Tanya anaendelea kueleza mengi kuanzia suala zima la baadhi ya makanisa kuendesha ibada zisizomtaja MUNGU mpaka suala zima la wenye nacho ambao kwa mtazamo wake wengi "hawana kazi" na suala la "wazazi watoto" na mengineyo
Bofya player hapa chini umsikie Tanya Stephens akielezea yale aliyochoshwa nayo na siku ambayo wengi twaitamani

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.

IJUMAA NJEMA

3 comments:

Simon Kitururu said...

Ijumaa njema kwako pia Alwatani!

Kamwesiga said...

Yawezekana ndo tunaelekea mwisho mwa dunia

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

alooo