Thursday, November 10, 2011

Happy EARTHday Mama P

Mama wa Changamoto. Mama awazishaye kwa sauti. Mama wa "behind the scene". Tangu enzi za wewe,.......
...mpaka enzi za sisi.....
..kisha nasi pamoja naye......UNAPENDWA TUUU!!!
Maisha ni zaidi ya yule tumuonaye, vile tumuonavyo na kwa yale tuyaonayo. Wapo waigizaji ambao maisha yao yaliyo nje ni tofauti na kilicho ndani. Wapo watu ambao fikra na maisha yao vimeharibiwa na wale waliopata kuwa nao ambao wamemuingiza katika maisha ya sasa. Na pia wapo ambao maisha ya sasa yanaendelea kugusa yale ya wengi kutokana na washauri ama watu waliowazunguka. Nami naamini maisha yangu yamekuwa mema ama bora zaidi kutokana na aliye msaada kwangu.
Wahenga walisema kuwa mafanikio ya mwanaume mara nyingi huja kwa msaada mkubwa wa mwanamke wake. NAMI NAKUBALI japo sikulazimishi kuungana nami.
Lakini kwa kila akubaliye ama kubisha katika kauli hii, ana haki ya kufanya hivyo na ni VEMA akawa na sababu za upande aliopo. Lakini si mashindano ya ukweli ama uongo wa kauli hiyo, bali uhalisia wa maisha yetu kwa namna yasongavyo.
Wenye kuchunguza wanajua, kuwa hata kama unamuona mtu mmoja mbele ya "screen" yako akitangaza, timu nzima inayoshiriki kukuletea matangazo hayo.
Basi kwenye hiyooo "behind the scene" ya maisha yangu ya sasa na yajayo, yupo DIRECTOR huyo mwenye taswira hapo juu.
Kama kuna kinachonifanya kusonga mbele nikiwa na tabasamu na tumaini basi ni mke wangu Mpeeenzi ESTHER. Ambaye amekuwa msaada mkubwa niwapo na uchovu wa kiImani, kimwili, kiakili na kiuchumi. Na leo tunakumbuka siku muhimu saana maishani mwake. Siku iliyoanzisha yote mema nijivuniayo maishani kutokana na uwepo wake. SIKU YAKE YA KUZALIWA.
Kama alivyoimba Beres Hammond, kuwa naye kunaifanya dunia isiwe na makali iliyonayo na kunanifanya niendelee kujiona niko "peponi". Msome ukisikiliza kibao chake STILL WILL BE HEAVEN

If i'll live to see a hundred years or so,
And the ocean is now where green trees used to grow,
If suddenly everything just disappear
No where to go, no friends to see, house isn't there.
But if i look around and you are by my side
Every step i'll take, i'll take them all with pride
I'll sure miss this world and all it's rights and wrongs
I'll miss all the fun and all the beautiful songs
But
STILL WE'LL BE HEAVEN AS LONG AS YOU'RE THERE........
Happy Birthdate my Love a.k.a Mama P.

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

HONGERA SANA KWA SIKU YA KUZALIWA MAMA P/WIFI NA MWENNYEZI MUNGU NA AKUBARIKI UWE NA NGUVU ZAIDI ILI UWEZE KUITUNZA FAMILIA YAKO PIA UWE NA AFAYA NJEMA. HONGERA SANA TENA.

Nefertiti said...

WOW...... Happy EarthDay Mama P. I give you Congratulations because you have EARNED a beautiful name from your dear Hubby - 'Mama P' it tells how accomplished you are in every womanly possible way.

I am your older sister in many ways...therefore am allowed to say the following....
1. Because you are not Pretentious or fake in every way - You will not receive Fake or made-up claims from Baba P...therefore...keep it up and Glorify the most high for creating you the way He did - Beautiful and Bountiful.
2. Pass on the values you uphold so graciously to beautiful Mtoto P - bila uchoyo au woga.

3. Never ever ever take your hubby's love and respect for granted !!! most women do make that mistake and eventually lose everything.

4. Don't forget to say a prayer for the distinguished Womb that brought you forth..... or the provider of the seed that became WONDERFUL, BEAUTIFUL YOU....Wife of our beloved brother BANDIO, Mother of our future 'Heritage Custodian' - Mtoto P, ...

In other words TUNAKUPENDA... MUNGU AKUBARIKI.
Dadio, Nefertiti.

Rachel Siwa said...

Hongera Wifi mamakeP,Mungu akubariki katika yote na undelee kuwa mama na Mke bora daima.

nuru said...

Hongera kwa siku ya kuzaliwa Mungu akubariki Mama P

Simon Kitururu said...

Hongera Mama P!

Mija Shija Sayi said...

Hongera sana mama P..

Ila Paulina amekua sasa jamani..

Happy Earthday.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hongera. kumbe tofauti na mama mwombe ya birthday ni siku nane tu?? sikujua mgesheherekea pamoja