Sunday, November 13, 2011

Za Kale vs Maisha ya sasa....BINADAMU HAWANA WEMA


Kama kuna kiumbe hatari duniani, basi ni kiumbe ambacho chaweza kuwa bora zaidi. Nacho ni BINADAMU. Ubaya na ubaya wa binadamu ni kutokana na uwezo wao wa kuonesha na kuvuta hisia na imani ya watu ambao si lazima awe ana nia aoneshayo usoni mwake mbele yao. Martin Luther aliwahi kusema kuwa binadamu anaweza kufanya ukatili ambao haudhaniki na hautendeki na kiumbe kingine chochote ulimwenguni. Anaweza kutenda kila awezacho kukuonesha anakuali ilihali anafanya juhudi mchana na usiku kukuondoa katika unyoofu wa maisha yako ikiwa ni pamoja na kukukatisha uhai wako. Sikilia kisa kiimbwacho naye Hassan Rehani Bitchuka akiwa na wana OSS katika wimbo huu Binadamu Hawana Wema** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia siku za Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

1 comment:

Unknown said...

Lakini mkuu si unafahamu kuwa kulikuwa na kasheshe kati ya Bichuka na Shaaban Dede...??? Ndiyo chimbuko hasa la wimbo huu...