Wednesday, November 16, 2011

Mazishi ya ndugu Nasibu Juma Manyala

Ndugu Watanzania,

Ndugu yetu Nasibu Juma Manyala
alifariki huko Michigan.Na sasa Powers of Attorney, ambayo ilikuwa
ikisubiriwa ili taratibu nyingine ziweze kukamilika, imekwishatolewa na
familia kwa Professor Deo Ngonyani wa Michigani ili aweze kusimamia
mazishi kwa taratibu za Kiislamu.
Mazishi yatafanyika siku ya Ijumanne tarehe 22.11.2011 huko huko Lancing
Michigan.
Ili kufanikisha mazishi haya ya ndugu yetu,tunaombwa kutoa michango yetu
ya hali na mali.

Unaweza kutuma fedha kupitia:
Nasibu Juma Manyala(Memorial Account)
MSU Federal Credit Union,
Memorial Acc#43380705 Routing#272479663
Au unaweza kuwakabidhi wafuatao:

1.Professor Deo Ngonyani-Simu 517-614-3543

2.Mussa Maingu-Simu 517-980-4444

3.Abbas Missana-Simu 202-378-8066

4.Dj Luke Joe-Simu 301-661-6696

Asanteni

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa Taarifa. Poleni sana kwa msiba. Mungu alitoa na Mungu amechukua. Marehemu na astarehe kwa amani mahali pema peponi. AMINA.

Simon Kitururu said...

R.I.P Nasibu Juma Manyala!