Waziri wa Ujenzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli
Moja kati ya habari zilizotawala mwanzo wa mwaka huu ni kupanda kwa nauli za vivuko na hasa cha Kigamboni. Hili limeonekana kupata msukumo wa upinzani toka sehemu mbalimbali na zaidi toka kwa WABUNGE walioonyesha nia ya kumfanya Waziri Magufuli awaombe radhi wananchi na pia kufuta kauli yake. Kauli inayozungumziwa hapa ni ile aliyonukuliwa akisema "Na
atakayeshindwa kulipa nauli mpya Dar- Kigamboni na apige mbizi au azunguke
Kongowe" Hii IMEWAKERA WENGI (miongoni mwa wachache waliolalamika)
Kwanza niwapongeze wabunge wa KULIVALIA NJUGA HILI.
Lakini pia niwapongeze kwa uwezo wao kuwahadaa wananchi wao juu ya hili.
Suala la kupanda kwa nauli linaonekana kutokea na kupata nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari kwa sababuni kweli kuwa WANANCHI HAWANA UWEZO WA KULIPIA KIVUKO (hata kabla ya nyongeza ilikuwa taabu)
Lakini lazima sote tukubali kuwa kuna ulazima wa kuongeza bei ya kuvuka kwa kuwa GHARAMA ZA KUENDESHA KIVUKO ZIMEPANDA.
Sasa hapa kuna namna ya kushughulika na haya. NAMNA AMBAYO WABUNGE WANGU (walio wabunifu wa kukwepa vyanzo vya matatizo) wanaepuka. Tunatakiwa kuangalia chanzo cha tatizo kuliko mvuto wa kuendekeza "UVIVU WA FIKRA" ambao unatuaminisha katika kila tunacholishwa na hawa wanajaribu kupata "UTENDAJI KAZI" kwa mambo ambayo si suluhisho la matatizo ya wananchi.
Na hili (la kutatua chanzo cha tatizo) ndilo la muhimu kuangalia kwa kuwa ndilo litakalotatua tatizo na pia limo ndani ya uwezo wetu.
Gharama za kuendesha kivuko si kitu ambacho tunaweza kushughulikia kwa urahisi. Lakini tunaweza kujadili na kutatua suala la uwezo wa wananchi kulipia kivuko hicho.
Majuzi niliona WARAKA WA KAKA MBUNGE WA KIGAMBONI kuhusu kupinga ongezeko. Na nukuu ya walionakiliwa. Nami palepale (kwenye facebook) nikampongeza na kumueleza "Hii ni safi sana. Naamini wananchi wa Jimbo lako wataanza kufuarahia MPANGO WAKO MPYA wa kuwawakilisha na kutuwekea hapa. Sijawa na takwimu halisi, lakini nilisikia "pingamizi kubwa" la wananchi wa Kigamboni kuhusu POSHO ZENU WABUNGE. Unaweza kuliandikia na hilo pia? Ama ni mimi niliyekosa barua yako kuhusu hili? HERI YA MWAKA MPYA" na yeye akanijibu akisema "Mubelwa acha fujo. Msimamo wangu ni kwamba mfumo mzima wa malipo kwa watumishi wa umma unapaswa kuangaliwa upya na usilenge wabunge peke yao."
Haikuniingia akilini kuona HOJA YANGU INATAFSIRIWA KAMA FUJO, na ndio maana nikamjibu kuwa "FUJO? Kaka. Nadhani unatania. Na kama la, basi nitalazimika kuanza kukushangaa. Ni kipi nilichosema ambacho ni cha fujo? Je! Kwa huo msimamo wako kuwa "malipo kwa watumishi wa umma unapaswa kuangaliwa upya na usilenge wabunge peke yao" ULIUANDIKIA BARUA KAMA HII? Kama ndivyo, pongezi. Kama sivyo, kwanini? Na hii pia inakuwa fujo?
Nahisi unanirejesha kulekule kwa Ndg Lazaro Nyalandu aliyelalamika kuwa sisi tuulizao hili na lile TUNA UBUNIFU WA KULALAMIKA. Sina hakika kama hili ni suala lililopo "mjengoni" ama la. Lakini kama nilivyoweka bayana MSIMAMO WANGU KWA NDG. NYALANDU HAPA, sitasita kuweka bayana kwa yeyote atakayeonyesha ubunifu wa kulalamikia walalamishi wasio wabunifu. "
Swali ni kuwa KWANINI WANANCHI WASHINDWE KULIPA? Na je! Magufuli akiomba radhi itasaidia vipi kubadili maisha ya wananchi?
Niliwahi kutoa mfano mmoja wakati nimekwenda Karagwe mwaka 2003. Wakati huo, rais wa awamu ya tatu alikuwa ametoa msamaha wa kodi ya wananchi. Watu wakapongeza. Lakini nilipokwenda kijijini Karagwe nikagundua kuwa WATU HAWAKUHITAJI MSAMAHA WA KODI KWANI HAUKUWA UKIWASAIDIA KUTATUA TATIZO LAO LA UCHUMI. Wakati huo, nilifika gulioni na kukuta watu wameleta mikungu ya ndizi ambayo walikuwa tayari kubadilishana nayo kwa PAKITI YA CHUMVI YA SHILINGI HAMSINI. NA HAWAKUPATA MTU WA KUBADILISHANA NAO. Wakaziacha hapo kwa kuwa hata nyumbani zipo zinazoivia shambani. Wakati huo huo, mkungu huo wa ndizi ulikuwa ukiuza kwa maelfu ya shilingi jijini Dar. TATIZO LILIKUWA NI BARABARA. Kama barabara ingekuwa nzuri, basi magari yanayofuata ndizi yangefika kule, na pengine wangeuza kwa shilingi elfu moja ama mbili, yule muuzaji angeuza mwanza kwa elfu kama tano na wale wa Dar wangeipata kwa bei zaidi.
Ina maana kama mtu huyu angeuza mikungu mitatu, angepata shilingi elfu tano za kulipa kodi. Kwa maana nyingine, mwananchi angelipa kodi, mwananchi angebaki na pesa mfukoni na serikali ingekusanya mapato zaidi na pengine mlaji wa Dar angepata ndizi kwa bei nafuu zaidi kwa kuwa usafiri usingekuwa na gharama kubwa sana.
Ni hilo linalonifanya niiwaze Kigamboni.
Wananchi hawana maisha mabaya kwa kuwa Magufuli kaongeza nauli, bali kwa kuwa WANANCHI HAWANA KAZI, HAWANA BIASHARA NA / AMA VYANZO VYA MAPATO.
Na hili ndilo liletayo yote haya. Na HILI HALITOKANI NA KAULI AMA HATUA YA MAGUFULI KUPANDISHA NAULI.
Hawa wabunge niliosikia wamemtaka Waziri Magufuli aombe radhi, wangeanza kwa kutueleza wao wamewafanyia nini wananchi wao kuweza kuwakwamua katika uwezo mdogo wa kulipa nauli? HILI NDILO TATIZO KUU.
Kama wananchi wangekuwa na kipato mara mbili ya walicho nacho, wasingejali kuongezewa hizo gharama, hasa kwa kuwa zimetajwa kuongezwa kwa NIA ILIYO SAHIHI. Suala la kauli ya Magufuli, ni moja, lakini haliendani na CHANZO CHA TATIZO.
Narejea kusema kuwa JAPO DALILI ZA KUKOSEKANA KWA MAJI KWENYE MTI HUONEKANA KWENYE MAJANI, WAKATI WA KUMWAGILIA, TUNAMWAGILIA MIZIZI NA SI MAJANI. Wabunge wajiulize kwanini wananchi hawataweza kulipa hicho kiwango kipya badala ya kung'ang'ania kuwa kauli ya Magufuli ni mbaya.
By the way, wangeshughulikia na kurejesha pesa zilizofujwa, wakagoma kupokea posho zao na kuacha ku-extend vikao kwa mambo yasiyo na tija kwa wananchi, ningeweza amini kuwa wana "uchungu na wananchi wao". Na pengine pesa hizo zingetosha kujenga daraja.
Nimeona wakilalamika kuliko ambavyo nilisikia wakiWAKILISHA MAONI YA WANANCHI KUHUSU POSHO ZAO, KUHUSU UMEME, KUHUSU MENGINE MENGI.
KABLA MAGUFULI HAJAOMBA RADHI....WABUNGE MTUELEZE MMEFANYA NINI KUWAWEZESHA WANANCHI KUMUDU (JAPO) NAULI YA ZAMANI, YA SASA (ILIYO NA ULAZIMA) NA PIA KUTIMIZA AHADI ZENU. Mtueleze MMEWAWAJIBISHA VIPI MAFISADI, na MNAONA UWIANO GANI KATI YA PESA MNAZOLIPWA, KAZI MNAYOFANYA NA WANANCHI WA MAJIMBONI MWENU!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Kaka, sina la kuongeza hapa, natamani wabunge na viongozi wengine wasome haya na wayafanyie kazi.
Post a Comment