Tuesday, February 14, 2012

Mahojiano kamili na Prof. Lipumba

Jumamosi ya Feb. 12, nilipata nafasi ya kuzungumza na mwenyekiti wa taifa wa chama cha Civic United Front (CUF) ambaye pia alikuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1995, 2000, 2005, 2010)
Mahojiano haya nimeyagawa kwenye sehemu tatu.
Katika sehemu hii ya kwanza, amezungumzia kilichomleta hapa nchini Marekani, hali ya siasa ndani ya CUF, kwanini chama chake kimepoteza mguso kwa wananchi, siasa za nchi na hata kujibu maswali toka kwa wasomaji mbalimbali waliouliza kupitia mtandao wa Facebook.

Katika sehemu hii ya pili, amezungumzia utata wa chama chake kuwa sehemu ya upinzani Tanzania Bara ilhali ni sehemu ya serikali Zanzibar, mambo yaliyo katika ilani ya CUF yaliyojumuishwa katika serikali ya Zanzibar, suala la chama chake kutoungana na CHADEMA kuing'oa CCM, na pia ni vipi tunaweza kuenzi umoja tukithamini u-Bara na uVisiwani. Mwisho anaeleza mambo ambayo CUF itafanya kuhakikisha kuwa Tanzania haiwi tegemezi wa misaada ya wahisani.

Katika sehemu hii ya tatu, anajibu swali iwapo atagombea urais mwaka 2015, anazungumzia kuhusu kitabu anachoandika kuhusu hali ya uchumi Tanzania, namna ambavyo serikali inawatumia wasomi kama yeye, msimamo wa chama cha CUF kuhusu Katiba ya Tanzania na mapungufu yake, maandalizi ya CUF kwa uchaguzi wa 2015, anajibu swali la kwanini wasiachane na urais na kugombea ubunge ili kuleta upinzani bungeni, nafasi ya mwanamke ndani ya CUF, nafasi ya upinzani kuiodoa CCM madarakani 2015 na NAMNA YA KUIBADILI TANZANIA.