Sunday, February 5, 2012

Mhe. Freeman Mbowe na ujumbe kwa DIASPORA

Jana, ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendelo uliokuwa hapa nchini ulifanya mazungumzo na waTanzania waishio vitongoji vya Washington DC.
Ujumbe huo wa Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye ni Mbunge wa jimbo la Hai na kiongozi wa upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe na Mbunge wa Nyamagana ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Ezekiel Wenje, ulianza kwa kueleza mambo mbalimbali yaliyowaleta hapa nchini na pia kutoa salaam ama ujumbe wa Chama kwa waTanzania waishio nje ya nchi. Msikilize HAPA

Baada ya salam zake zilizotanguliwa na zile za Mhe Wenje, ukafika wasaa wa maswali na Majibu ambapo wananchi waliohudhuria walipata fursa ya kuuliza mambo mbalimbali kuhusu Chadema na Tanzania kwa ujumla. Moja ya maswali yaliyoulizwa ni namna ambavyo Chadema inalichukulia suala la mgomo wa madaktari unaoendelea kuathiri huduma za afya nchini Tanzania. Mhe Mbowe analijibu hilo HAPA ambapo pia anaeleza namna ambavyo uoga wetu unakwamisha harakati za kuishinikiza serikali kufanya mabadiliko yatakayoifaa jamii.

Swali jingine lililoulizwa lilikuwa ni juu ya tatizo za utawala wa sheria kwa wote, juu ya matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo nchini na mchakato wa uraia wa nchi mbili ambayo yalijibiwa kama yasikikavyo HAPA

Likaja swali toka kwa mwanamama aliyemtaka Mwenyekiti Mbowe afafanue tetesi ama shutuma kuwa Chadema ni Chama cha waChagga. Hapa
anafafanua dhana zote hizo na ile aliyosema iliwahi kusambaa kuwa ni "chama cha waKristo"
Msikilize

Pia likaulizwa suala la namna ambavyo Tanzania inaweza kuondokana na utegemezi wa nchi wahisani katika bajeti yake. Hapa
anajibu swali la jinsi ambavyo anaamini Chama chake kinaweza kuondoa utegemezi wa misaada ya nchi wahisani

Lakini pia alizungumzia namna ambavyo tunastahili kuondokana na zile fikra za malighafi na kuanza kuwekeza katika "maliwatu"
Mzikilize hapa chini alivyoichambua


Panapo majaaliwa, mwishoni mwa juma hili tutafanya mahojiano na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF). Kama una swali ambalo ungependa kumuuliza, basi shiriki nasi hapa, ama kupitia changamoto at gmail dot com.

Photo Credits: Abou Shatry wa Swahilivilla blog

No comments: