Friday, May 25, 2012

CHADEMA USA TOUR

Ujumbe wa Mhe. Zitto Kabwe kuhusu mkutano huu katika ukurasa wake wa Facebook unasema
 "Kesho Jumapili tarehe 27 Mei mwaka 2012 nitakutana na Watanzania wanachama na wapenzi wa CHADEMA wanaoishi Marekani. Mkutano utafanyika katika Jimbo la Maryland kama ilivyokwisha tangazwa hapo awali.
 Katika mkutano huu wa kwanza na wa aina yake tutazindua uandikishaji wa wanachama wa CHADEMA kwa Watanzania wanaoishi Marekani. Pia tutazungumza masuala mbalimbali yanayohusu nchi yetu. Masuala ya kwanini nchi yetu haiondokani na umasikini licha ya utajiri wa rasilimali uliopo nchini, masuala ya namna gani tunajiandaa na uchumi wa gesi asilia na nafasi ya Watanzania waishio nje katika maendeleo ya Taifa.
 Tutazungumza kuhusu uandikaji wa Katiba mpya na namna haki za Watanzania wanaoishi nje zitakavyoingia kwenye Katiba ikiwemo haki ya kupiga kura na hata haki ya kuwa na Uraia wa pili.
 Ninapenda kuwakaribisha katika mkutano huu muhimu sana. Njooni tuzungumze. Njooni tujadiliane. Wasiliana na viongozi wa chadema Marekani kwa maelekezo zaidi."

No comments: