Monday, June 4, 2012

Katika "kupotea" kwangu

Kama nilivyosema awali, kulikuwa na "muadimiko" wangu hapa/ Lakini katika muadimiko huo, kukawa na pilika mbalimbali.
Lakini kati ya niliyofanikisha ni kupata mahojiano na baadhi ya watu, na zaidi wanasiasa.
Kwanza nilihojiana na Katibu Mkuu Msaidizi wa CHADEMA ambaye ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Katika sehemu hii ya kwanza, Mhe Zitto Kabwe anazungumzia hali ya kisiasa ndani ya CHADEMA na TANZANIA. Hofu yake juu ya ukuaji wa chama chake. Matatizo yanayoukumba uchumi wa nchi. Je! Anahofia kuwa yale yaliyotokea kwenye nchi za Arabuni yanaweza kutokea Tanzania? Kwanini anasema kuna tatizo la uwajibikaji nchini Tanzania? Anafafanuaje hoja hii? Ni ipi silaha ya mwanasiasa wa Tanzania? Na kwanini anaamini kuwa imepotea? Suala la KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU. Ilikuwaje, ikoje na nini kinafuata? Je! Baada ya kubadili baraza la mawaziri, HOJA IMEKUFA? TATIZO LA AJALI... Kwanini maelfu ya wananchi wanakufa ajalini na hakuna kiongozi anayeonekana kujali ilhali akihusisha Waziri ama M'bunge mmoja nchi nzima inazizima? Kwanini serikali haiarifu wananchi kama inavyostahili na mengine mengi Katika sehemu hii ya pili iliyozungumza TANZANIA KUELEKEA 2015, Mhe. Zitto Kabwe anazungumzia kuhusu NIA YAKE YA KUWA RAIS, Msimamo wa Chama na wake kuhusu Muungano, suala la CHADEMA kuondoa kinga ya kikatiba kwa Rais, anaeleza kwanini anaamini ni vema uchaguzi wa Rais na Wabunge vitenganishwe, haki na wajibu wa raia katika katiba, kilichotokea Mwanza kwenye vurugu zilizosababisha wabunge kushambuliwa na kujeruhiwa na mengine mengi. Katika sehemu hii ya tatu iliyojikita katika MAHITAJI YA TANZANIA, Mhe. Kabwe anazungumzia mashirika ya umma nchini Tanzania. Je! Yapo kwa faida ya wananchi? Kama Mwenyekiti wa Tume ya Mahesabu ya Mashirika ya Umma anazungumzia vipi tatizo la TANESCO? Ni nini kilisababisha TANESCO kufikia lilipo? Vipi wanajizatiti kuondoa hasara iliyokumba? Ni vipi wana-diaspora wanaweza kushiriki katika kufufua Tanesco?+ Ni wapi pa kuwekeza nchini? Ukuaji wa miji na suala la mipango miji. Kufuta vyeo vya wakuu wa mikoa na wilaya. PIA..KWANINI KILIMO NDIO UTI WA MGONGO JAPO UNAZALISHA ASILIMIA ASILIMIA NDOGO ZAIDI NCHINI? Ni vipi Tanzania inaweza kuondoka katika umaskini kwa muda mfupi? na Je! ELIMU YA TANZANIA....INAKUA AMA INAPOROMOKA? INAIFAA JAMII YA TANZANIA? Katika sehemu hii ya nne iliyozungumzia MUSTAKABALI WA TANZANIA, Mhe. Zitto Kabwe anaeleza kwanini anaamini kuwa TANZANIA NI NCHI TAJIRI SANA? 1: Anauonaje MUSTAKABALI WA TANZANIA hasa katika nyanja ya mafuta na gesi? Je! Tanzania ina gesi kiasi gani? Ni mikataba gani iliyosainiwa na hiyo ina tofauti gani na ile ya zamani? Ni nini serikali inapanga kufanya na pesa za madini? 2: Suala la mipango miji kwa maeneo yanayokua 3: Tatizo la usafiri na miundombinu kwenye miji kama Dar-Es-Salaam 4: Tatizo katika mfumo wa Magereza na haki za wafungwa. 5: NI KIPI AMBACHO CHADEMA WANAJIVUNIA KAMA MATOKEO YA HARAKATI ZAO NCHINI?

No comments: