Thursday, June 7, 2012

WITO: Kikao juu ya hali ya mTanzania aliye hospitali

Kwanza tunapenda kuwashukuru wote walioshirikiana na familia kukutana na hata kuwasiliana nasi kuhusu kikao kilichotangazwa kufanyika Jumatano iliyopita (tarehe 30 Mei). Kilifanyika kama ilivyopangwa na tunashukuru kwa wote waliohudhuria na wale ambao waiwasiliana nasi kabla, wakati na baada ya kikao kueleza kushindwa kuhudhuria. Mpaka hivi sasa hali ya mgonjwa ilikuwa ikiendelea vema zaidi na hadi kufika siku ya kikao, alikuwa ameondolewa hata dawa za maumivu makali alizokuwa akitumia. Baadhi ya maendeleo yaliyopatikana mpaka sasa ni pamoja na kushiriki katika njia tofauti kuisaidia familia ya Bwn. Domitian Rutakyamirwa hasa mke na watoto. Hii ni pamoja na mchango ambao ulikusanywa toka kwa watu mbalimbali kusaidia gharama za matunzo ya mgonjwa na baadhi ya gharama za familia yake. Pia, kuna akaunti maalum iliyofunguliwa kwa ajili ya kusaidia gharama kwa familia Jina ni….
DOMITIAN CARE AND SUPPORT ACCOUNT.
Benki…. BANK OF AMERICA
Routing.. 052001633
Account.. 446026881993.

Bado Ndg Domi (kama anavyojulikana kwa wengi) anahitaji maombi pamoja na dua ili Mwenyezi Mungu aweze kumuangazia. Amelazwa chumba namba 523 katika hospitali ya Chuo Kikuu cha George Washington iliyopo
900 23rd St., NW.
Washington, DC 20037.
Pamoja na maombi, Ijumaa ya wiki hii (June 8, 2012), familia ya Ndg Domi itakutana na ndugu, jamaa na marafiki kujadili masuala kadhaa kuhusu hali yake. Unakaribishwa kuhudhuria na kutoa mchango wako wa mawazo katika yale yatakayojadiliwa.
Kikao kitafanyika saa moja kamili jioni. Anwani ni
10110 Greenbelt Rd,
Lanham,MD,20706

 NYOTE MNAKARIBISHWA

Unaweza kuwasiliana na
Henry Kente: 240-938-2452
Bernadetha Kaiza: 240-704-5891
 Mubelwa Bandio: 240-281-0574

No comments: