Friday, August 31, 2012

Mhe. Mbowe na Mhe. Mbilinyi kukutana na waTanzania DC

Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Tawi la Chadema DMV, unawakaribisha waTanzania wote kuhudhuria mkutano utakaofanyika Siku ya Jumamosi Spet 1,2012.
Mkutano huo utaaza  rasmi saa  Kumi za Jioni

 Wageni rasmi kwenye mkutano huo watakuwa Mhe. Freeman Mbowe ambaye ni kiongozi wa upinzani bungeni na Mhe Joseph Mbilinyi
Anwani ya mkutanoni ni
9670 Baltimore Ave. 
 College Park. MD 20740
 Nyote Mnakaribishwa

NB: Chakula vinywaji Bure
 

1 comment:

Mbele said...

Mimi ni m-Tanzania ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Isipokuwa, kutokana na jinsi CCM ilivyohujumu na inavyoendelea kuhujumu mapinduzi tuliyoanza nayo wakati wa TANU, na hasa hasa kwa vile CCM, kwa kuhujumu Azimio la Arusha, imetuletea janga la ufisadi, naegemea upande wa CHADEMA, chama ambacho kinahamasisha mapambano dhidi ya ufisadi, mapambano yenye lengo la kuzuia uporaji wa rasilimali za Tanzania. Niko huku Minnesota, ila ningekuwa upande huu wa Washington DC, ningehudhuria mkutano huu, kuiunga mkono CHADEMA.