Sunday, September 2, 2012

R.I.P Kaka David Mwangosi

Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Bwn. Daud Mwangosi 
Nimesoma kuwa mwanahabari mwenzangu David Mwangosi ameuawa kwenye vurugu kati ya Polisi na wafuasi wa CHADEMA. Amefia kazini
Kwa wale wenye fikra fupi kuhusisha,......kilichomkuta Kaka yetu ni sawa na ....
Rais kuuawa Ikulu.
Askari kuuawa vitani.
Mbunge kuuawa bungeni.
Daktari kuuawa chumba cha upasuaji.
Mtangazaji kuuawa studio.
Mkulima kuuawa shamba.
Mwalimu kuuawa darasani.
Ukisoma orodha hiyo, utagundua kuwa japo wote watakuwa wamekufa wakitekeleza majukumu yao, wapo watakaothaminiwa zaidi ya wengine kwa kuwa TUMEJENGA MATABAKA YA KAZI.
R.I.P Brother Mwangosi 

LAKINI NILIANDIKA HAYA MIAKA 3, MIEZI 2 NA SIKU MOJA KABLA YA KUUAWA KWA MWANDISHI MWENZANGU Bwn. DAVID MWANGOSI

Niliipa kichwa kisemacho TUNATAKA KUWAAMINI POLISI, LAKINI HAWAAMINIKI.
"Kuna matukio mengi yanayotendwa na askari polisi nchini ambayo yanasikitisha saana. Hatujui ulipo mstari kati ya usalama wa raia na siasa.
Kumekuwa na mambo mengi ambayo yanapunguza heshima na imani ya wananchi kwa jeshi hili. Kibaya zaidi ni kuwa Polisi HAWAAMINIKI katika yale watendayo. Si tunakumbuka yaliyotokea wakati wa mauaji yaliyoanzisha kesi ya kina Mhe Zombe?
Tuliambiwa nini na tukaja kugundua nini? Unadhani watu wanafikiriaje kuhusu jeshi lao?
TUMESHUHUDIA wasio na hatia wakihukumiwa, wakiuawa na hata kusingiziwa mambo mbalimbali. Unafika wakati WANANCHI WANAKOSA IMANI, UPENDO NA HESHIMA kwa jeshi hili na kuamua kujichukulia hatua mkononi.
Hili si jambo jema hata kidogo lakini badala ya kujitahidi kuwatisha na kuwafunga wasio na hatia, JESHI LA POLISI LIBADILI, LIBORESHE NA KUHESHIMU UTENDAJI WAKE WA KAZI NA KUTENDA HAKI KWA WANANCHI"


Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA


Tuonane "Next Ijayo"