Sunday, September 2, 2012

Tanzania ni zaidi ya itikadi- Benjamin Mwaipaja

 Katibu Uenezi na Itikadi wa CCM-DMV Bwn. Benjamin Mwaipaja (kati) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA TAIFA Mhe. Freeman Mbowe. Kushoto ni Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi
Kada wa Chama Cha Mapinduzi Bwn Benjamin Mwaipaja, amewaomba wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa kuweka utaifa juu ya itikadi zao katika kuhakikisha kuwa nchi yetu inasonga mbele.
Katibu Uenezi na Itikadi wa Tawi la CCM DMV Benjamin Mwaipaja akiwa na Kada wa Chadema Mzee Emmanuel Muganda katika mkutano huo.
Akizungumza na blogu hii punde baada ya kuhudhuria mkutano ulioandaliwa na tawi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) la Washington DC, Bwn. Mwaipaja, ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CCM tawi la Washington DC amesema kuwa licha ya tofauti za itikadi zilizopo baina yetu, sisi wanaDiaspora tunastahili kukumbuka kuwa tuna wajibu wa kuijenga Tanzania BORA NA IMARA kwa manufaa yetu, ndugu zetu walio nyumbani sasa na vizazi vijavyo.
Sikiliza mahojiano yangu na Ndg. Mwaipaja HAPA chini
Katika mkutano huo uliofanyika jana usiku katika kitongoji cha College Park jimbo la Maryland Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi na Mbunge wa Hai ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe walihudhuria.
PHOTO CREDITS: Abou Shatry wa SWAHILI VILLA BLOG

1 comment:

emuthree said...

Labda kuna kuongea na kutenda kisiasa, maana nakumbuka swali moja tuliulizwa tukiwa sekondari, lilisema;

'Siasa ni uongoo wenye ukweli ndanii yake, jadili.

Huenda ukaona swali hili linaibeza siasa,lakini huenda nia na lengo lamuulizaji ni kutaka kutafakuri siasa katika maana yake, na siasa kwa mtizamo wa wanasiasa, ambao wanaitumia hiyo siasa katika kukidhi matakwa yao!