Wednesday, August 22, 2012

Rushwa inapopingwa kinafiki.....Ujinga mwingine Washington DC..

Photo Credits: Steve Miller Blog
Siku za karibuni kumetokea MAMBO YA AJABU SANA HAPA WASHINGTON DC. Lakini hili la sasa ndio limesikitisha zaidi.
Nimesoma HABARI HII iliyoandikwa na "MWANAMAENDELEO WA DMV" ambaye licha ya kuwa na UWEZO MDOGO WA KUANDIKA, BADO AMEDHIHIRISHA UWEZO MDOGO WA KUJENGA HOJA. Mwana maendeleo huyu wa DMV ambaye hapendi jina lake lijulikane amechefua kwa kusambaza habari hiyo kwenye blog ambazo hazihudumii jamii inayolalamikiwa.
Nimkumbushe huyu MWANA MAENDELEO ambaye hana maendeleo katika kuandika baadhi ya mambo ambayo kwa hakika yanalifanya hili andiko lake lisiwe na "mashiko"
1: Haijulikani mwandishi ni nani (japo anajiita mwana maendeleo)
2: Amesema "WANASHUTUMIWA NA WANAJUMUIYA WA WASHINGTON KWA KUPOKEA RUSHWA KUTOKA KWA CHAMA CHA CHADEMA KWA AJILI YA KUFANYIA PICNIC NA PARTY YA USIKU..." Hao wanajumuiya ni idadi gani na walijumuika wapi kukusanya malalamiko yao?
3: Amesema "WAKEREKETWA WA JUMUIYA WAMEIPA MAMLAKA KAMPUNI YA ERNEST & YOUNG KUFANYA INDEPENDENCE AUDITING YA JUMUIYA ILI KUJUA INCOME AND EXPENDITURE ZA JUMUIYA HIYO ZIMETOKA WAPI NA ZIMETUMIKA VIPI..." Hao wakereketwa wanaotajwa hapa ni kina nani na kwanini wakereketwa wote ni ANONYMOUS
4: Katika sehemu ya mwisho ya maelezo yake ya kusikitisha, huyo mwana maendeleo amesema "HABARI ZA KUAMINIKA NA USHAHISI UPO ZINASEMA KUWA KATIBU WA JUMUIYA BWANA AMOSI CHEREHANI NI MWEKA HAZINA WA CHADEMA WASHINGTON NA NDIYE AMBAYE AMEWEZA KUHAMISHA PESA HIZO KUTOKA CHADEMA ILI ZIWEZE KUFANYA HAFLA HIYO.WANANCHI WANAHOJI KWA NINI MWENYEKITI AMBAYE ALICHAGULIWA KWA KISHINDO AMEWEZA KUKUBALI SWALA HILI WAKATI JUMUIYA HAIFUNGAMANI NA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA?....WAKEREKETWA WA JUMUIYA WAMEIPA MAMLAKA KAMPUNI YA ERNEST & YOUNG KUFANYA INDEPENDENCE AUDITING YA JUMUIYA ILI KUJUA INCOME AND EXPENDITURE ZA JUMUIYA HIYO ZIMETOKA WAPI NA ZIMETUMIKA VIPI KABLA YA HATUA ZAIDI KUCHUKULIWA...WANAJUMUIYA TUNAOMBA KUITISHA MKUTANO NA KUPIGA KURA ZA MAONI YA KUWA NA IMANI NA UONGOZI KWANI BADO NIMCHANGA NATULIUCHAGUA KWA IMANI HATUTAKI VYAMA VYA SIASA VITUINGILIE...RUSHWA NI ADUI WA HAKI!"
Kwani hapa tatizo ni party ama muingiliano wa tarehe na uzinduzi wa tawi la CCM hapa?
Nafurahi kuona kuwa si viongozi wa jumuiya wala wa CHADEMA waliojibu UTUMBO huu kwa kuwa hii ni sawa na kumkimbiza taahira aliyechukua nguo zako ukiwa uchi.

Na huu ni mtazamo wa namna nionavyo tatizo.
Labda namna nionavyo tatizo ndio tatizo.

No comments: