Thursday, August 23, 2012

SOTE NI NDUGU......Innocent Galinoma

"We share the same BIOLOGY regardless of our ideology. What we really wanna see is LOVE AND UNITY" Luciano
Ndivyo anavyonukuliwa Luciano katika wimbo wake MANKIND ambao amehimiza kutambua undani wa mtu ambao HAUTOFAUTIANI baina ya binadamu. Hili lina umuhimu saana kulitambua kwani ni SULUHISHO kwa matatizo mengi "ya hiari" tuyaonayo sasa. Kutambua kuwa SOTE NI SAWA kutatufanya tujiulize maswali mengi juu ya dhamira ya KUMTESA AMA KUMNYANYASA mwenzako.
Kama binAdam wangetambua kuwa tu wamoja, tu sawa, tu ndugu, basi tutafikiria MAUMIVU wanayopata wenzetu na kuacha kufanya hivyo kwani tutahisi twafanyiwa sisi.
Na kwa Tanzania huu ni mwaka wa sensa ambayo tumeambiwa kuwa NI KWA MAENDELEO YA TAIFA. Mwaka ambao tunastahili kuweka maslahi ya nchi na wananchi mbele katika kuhakikisha kile kilichodhamiriwa kwetu kinaweza kupangwa kwa kuwa tunajulikana idadi na mahitaji yetu. Huu ni mwaka ambao tunatakiwa kupata idadi kamili (ama idadi iliyo karibu na kamili) ili kuwafanya wale viongozi wanaotuwakilisha kutatua matatizo na mahitaji halisi ya mwananchi ambaye hawezi kuonana na wenye mamlaka ama uwezo wa kutoa suluhisho. Hili si jambo dogo na si jambo rahisi pia.
Tuna watu ambao (kwa mtazamo wao wa nje) wanaamini kuwa tofauti na wenzgine. Watu ambao wanaweza kujitofautisha na wenzao kwa vitu vya nje kama DINI, RANGI, UMRI, KABILA, MUONEKANO na mengine mengi yasiyotutofautisha ki-uhalisia.
Sisi soote ni waTanzania. Sisi sote tuna mengi makubwa ambayo yanatuunganisha na pia ni muhimu zaidi kuona tunavyounganishwa kuliko tunavyojiaminisha kuwa tunatenganishwa.
Picha na muziki kwa hisani ya INNO
Ni hapa ninapojikuta nagota katika wimbo wa Kaka Innocent Galinoma Mfalingundi ambao aliuimba miaka kadhaa iliyopita. Humo amehimiza huu umoja tunaostahili kuutambua kuwa SOTE NI NDUGU.
Amefunza kilichotokea tangu "enzi za mababu" ambako ameendelea kusema "watu tuliishi pamoja kama ndugu. Leo mambo yamegeuka hujui wa kumwamini. Rafiki yako mkubwa aweza kuwa adui, adui yako mkubwa aweza kuwa rafiki"
Ameeleza namna ambavyo UKOLONI umetuaminisha kuwa sisi si watu wamoja. Umetugawa (ili kututawala) na makombo ya akili hizo yakingali yanatutafuna leo hii kwa watu kuuana kwa tofauti ndogondogo.
Lakini haishii kutueleza hali ilivyokuwa na ilivyo sasa, bali anaendelea kutuhimiza kuwa "sisi sote ni ndugu, watoto wa Baba mmoja". Anazungumzia namna ambavyo dini, rangi, na vingine vingi vioneshavyo muonekano wa nje visivyo na nafasi katika maisha yetu.
Waweza kumtembelea Inno na bendi yake katika tovuti yao HAPA (ukifika huko usisite kusikiliza wimbo wa United States of Africa ulioimbwa mwanzoni mwa miaka ya 90 lakini watufaa leo kuliko wakati mwingine wowote).
Msikilize Innocent Galinoma katika kibao chake SOTE NI NDUGU.
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

1 comment:

emuthree said...

Umenena vyema mkuu, nami ndipo nakajiuliza, kwanini ilikuwa hivyo, maana nilipoanza kusoma kwenye fomu ya kujiunga shule, kuna kipengele kinauliza;
Jina lako, na mara dini yako...kwanini

Nilipoajiriiwa halikadhalika, kabila,mara jina lako , mara dini yako, ....kwanini, ...Haya kwenye vitambulisho, ni halikadhalika,kwanini...

Sisi sote ni ndugu na tafifa moja, katika maisha yetu ya kila siku ambayo yanamgusa kila mtu, hiki kipengele, cha kabila na dini yako, kisiwepo,ili ilete mantiki mena.

Mimi nionavyo, sio mbaya katika sensa,, wakaweka hivyo vitu, hiyoo ni kwa mtizamo wangu binafsi,kama sasa imeshindikana lakini tuagalia baadaye,..Maana hii ni nafasi pekee ambayo kila mtu anapitiwa, anaweza akaelezea jina lake, kabila lake, dini yake,nk.

Hii itasaidia kwenye kumbukumbu zetu,li kujua kabia fulani wapo wangapi, dini fulani wapo wangapi...katika takwinu zetu, hivi niulize watu wanajuaje kabial fuani wapo wangapi? sijui lini sensa ya kabila ilipitishwa, inakuwa kwa kukisia tu...
Ila kwa angalizo, iwe kwa nia njema kabisa. Maana hili ni zoezi ni kubwa,na lina gharama , na ndipo sehemu ambapo tunaweza tukapata kumbukumbu nzuri za baadaye. Ina maana hata hili tutasubiri mpaka wafadhili waje,wagundue kabila fulani wapo wangapi, ...hii ndio nafasi pekee,na muhimu,tuache mambo mengine ya hisia zetu.

Mimi hili silioni kuwa lina matatizo, kama tukiondoka hisia za `umimi'...
Ni wazo langu tu mkuu.