Wednesday, August 1, 2012

VODACOM......Hata ninyi?

Wiki iliyokamilika, kampuni ya simu ya VODACOM imetoa tuzo kwa bloggers kadhaa katika kuthamini mchango wao kwenye fani hii.
Katika orodha hiyo, sina shaka na yeyote aliyeshinda kwa sababu kuu mbili.
1: Wote wa walioshinda wanatenda kazi na kazi zao zina mafanikio kuliko blogu hii.
2: Sijajua ni vigezo gani vilitumika kupata washindi.
Lakini kama ambavyo niliandika mwaka jana wakati wa kusaka TUZO ZA BLOG BORA TANZANIA, kuna umuhimu wa watu kujua kwanini wanashinda na ama / kushindwa katika mchakato wowote.
KATIKA HILI....HAIKUJULIKANA. Nilisoma habari za tuzo hizi siku zilipotolewa na nikawaza baadhi ya mambo ambayo niliwaza wakati wa tuzo za awali za blogs.
Niliandika HAPA kwamba "KABLA HATUJAWA NA TUZO ZA BLOGU BORA tutekeleze ambayo naamini ni muhimu KUWEKANA SAWA kwa wateua na wateuliwa. Naulizia ama kuelezea VIGEZO kadhaa. 
-Kwanza BLOGU NI NINI? Na ni vipi tunaweza kuziunganisha ama kuzitenganisha na "forums" mbalimbali kama Jamii ama Wanabidii? 
-BLOGU ZINA JUKUMU GANI na ZINAWAFIKIA VIPI WALENGWA? Ni kweli kuwa blogu zetu zinajipenyeza kuelekea kwenye uhitaji? 
-BLOGU ZINATHAMINIKA kwa umaarufu wa wamiliki ama maudhui kwa jamii? 
-UBORA WA BLOGU NI UPI? Idadi ya watembeleaji? Kama ndivyo basi Ze Utamu yaweza kuwa blogu bora zaidi kupata kutokea kwa waTanzania. Ama ni MAUDHUI yenye kuifaa jamii? 
-UPI UELEWA WA WATEUZI? Wateuzi watakaoteua ni bloggers ama wasomaji? 
KATIKA ORODHA ILIYOTOLEWA...... 
Ningependa kuona TUZO YA HESHIMA KWA KAKA NDESANJO MACHA. Muasisi wa blogu za kiswahili na ambaye anaendelea na mambo ya tovuti katika kukikuza na kukiendeleza kiswahili..."
NIACHANE NA MENGINE...nirejee kwa Kaka Ndesanjo Macha.
Kwa VODACOM kushindwa kuthamini mchango wa yule aliyefungua njia kwa maelfu ya bloggers nchini ni JAMBO LA KUSIKITISHA JAPO SIO LA KUSHANGAZA.
Kwa Tanzania yetu, tuna watu wengi waliofungua njia kwenye MUZIKI, UTANGAZAJI, UIGIZAJI na fani nyingine nyingi lakini hawathaminiki kwa kuwa wakati muafaka wa kuwaenzi HATUWAENZI.
Blogu hii imekuwa ikiandika kuhusu umuhimu wa kuwathamini waliofungua njia katika fani mbalimbali.
August 2008, tulibandika HAPA swali NI LINI TUTAWAENZI WATU HAWA? Na hii ilikuwa ni kwa ajili ya waasisi wa muziki. Miezi mitatu baadae tukaweka bandiko jingine HAPA kuhusu watu ambao HATUWATHAMINI KWA KUWA HATUWAJUI, mwaka uliofuata tukaweka bandiko HILI kuhusu TANZANIA YANGU...INAYOPUUZA HALL OF FAME NA KUTUKUZA HALL OF SHAME ambalo lilitoka miezi mitano baada ya HILI lililosikitisha habari za walezi wetu katika tasnia ya HABARI ambao TUNAWAPENDA, HATUWATHAMINI KWA KUWA HATUWAJUI
Kwa hakika VODACOM mmesikitisha kwa mlichofanya.
Mmeshakuwa na mkilalamikiwa na baadhi ya bloggers juu ya udhamini wenu kwenye blogu mbalimbali.
Mnajali IDADI YA WATEMBELEAJI hata kama baadhi ya blogu mnazodhamini ZINADHALILISHA na zimejaa MATUSI.
Naungana na Kaka Bonny Makene katika alilosema HAPAkuhusu tuzo hizi.
KWA UJUMLA......NILITEGEMEA VODACOM MNGEFANYA MCHUJO MZURI NA KUSAIDIA KUTHAMINI WALIOONYESHA NJIA, KUTOA CATEGORIES MLIZOFUATA NA KISHA KUWAELEZA WENZETU WANAOFANYA KAZI NZURI YA KU-BLOG WAWEZE KUSHIRIKI.
Na huu ni mtazamo wangu kwa namna nionavyo tatizo.
Labda NAMNA NIONAVYO TATIZO NDIO TATIZO

2 comments:

emuthree said...

Mimi nilipoona tangazo lao nilisema kuwa `mwenye nacho ataongozewa' na huenda ni moja ya kulipa fadhila za kuzitanagza biashara zao, sina uhakika na kusudio jingine.
Huenda ni mwanzo kwao , huenda wana malengoo zaidi, lakini ...ni vyema wenye blogs wakajua nini hasa wanachokihitaji kwa blogs,ili iitwe bora!

Unknown said...

kwa kampuni kubwa kama hili mimi nilitegemea ingekuwa nzuri sana lakini kinyume chake ni kwamba ni afadhali hata TBA (Tanzanian Blog Awards) kwa kile walichokifanya kushirikisha wasomaji ndivyo nilivyotegemea kwa Vodacom wangeandaa vipengele (categories) wangetangaza ili watu wapendekeze washiriki (nomination)na hatimaye namna za kupiga kura zingetangazwa kwa vile ninaamini kuwa anayeteuliwa na kuchaguliwa na wengi ndiye mshindi halali, nimependa uchambuzi wako Kaka Mubelwa na hilo changamoto Vodacom wanapaswa kuzingatia sana