Monday, September 3, 2012

Bin'Adamu....apumzikaye kusherehekea SIKU YA KAZI

Photo Credits: St Thomas Aquinas Pack 7 
Ni SIKU YA KAZI. Ama niseme kuthamini kazi. Ama siku ya wafanyakazi. Lakini vyovyote iwavyo, ni siku ambayo wengi wetu hapa Marekani tunakuwa na "siku ya mapumziko".
NDIO, DAY OFF katika kusherehekea SIKU YA KAZI.
Mmmmmhhh!!!
Umeona eeee?
Nilishaandika kuhusu kinyumenyume cha Bin-adamu katika kutenda, kunena na kuwaza. Kuwa kwanini tuwazishwe vitu kwa namna nyingine?
Kwanini nchi nyingi Afrika zisherehekee UHURU kwa staili ya gwaride kama la WAKOLONI WALIOTUTAWALA?
Kwanini siku ya wakulima isherehekewe mjini, na wapatao "day off" ni wale wasio wakulima ilhali wakulima hawapati sherehe yoyote siku hiyo?
Ni kwenye muendelezo huu wa KWANINI, najikuta naleta MASWALI YAFUATAYO, ambayo nilitumiwa na rafiki yangu, na si mawazo yangu.
TUMUWAZE BIN'ADAM NA UNAFIKI WA MAWAZO YA KIMATENDO.
Soma kisha uwaze, "bin'adamu anawaza nini kutenda atendayo?"
Japo nilitumiwa NICHEKE, lakini yaliniwazisha pia

-Why do supermarkets make the sick walk all the way to the back of the store to get their prescriptions while healthy people can buy cigarettes at the front?
-Why do people order double cheeseburgers, large fries, and a diet coke.
-Why do banks leave vault doors open and then chain the pens to the counters.
-Why do we leave cars worth thousands of dollars in our driveways and put our useless junk in the garage.

EVER WONDER .......
-Why the sun lightens our hair, but darkens our skin?
-Why can't women put on mascara with their mouth closed?
-Why don't you ever see the headline 'Psychic Wins Lottery'?
-Why is 'abbreviated' such a long word?
-Why is it that doctors call what they do 'practice'?
-Why is lemon juice made with artificial flavoring, and dish washing liquid made with real lemons?
-Why is the man who invests all your money called a broker?
-Why is the time of day with the slowest traffic called rush hour?
-Why isn't there mouse-flavored cat food?
-Why didn't Noah swat those two mosquitoes?
-Why do they sterilize the needle for lethal injections?
You know that indestructible black box that is used on airplanes? Why don't they make the whole plane out of that stuff?!
-Why don't sheep shrink when it rains?
-Why are they called apartments when they are all stuck together?
If flying is so safe, why do they call the airport the terminal?

HIVI TUNAWAZA NINI?

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya. Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***

1 comment:

emuthree said...

Mkuu, umewaza nini kuwaza hili, na mimi nimewaza nini kuwaza nini ulichoawaza wewe, ni maajabu ya ubongo,zawadi muhimu, aliyotupa mweneyzimungu,na huenda tumeshindwa kuutumia ipasavyo.

Unajua mkuu, nimegundua jambo, huenda wengine walishagundua, na wengine watabeza, lakini ukichunguza kwa undani utagundua kuwa kuna ukweli ndani yake.

Kila jambo unaloliona linafanyika, lilishakadiriwa,...swali ni nani , kwa kifupi tunaweza kusema ni makadrio ya Mungu au ? na ukienda mbali zaidi huenda tukasema ni makadrio ya wanadamu wajanja...hapa akili kichwani kwetu.

Kuna mtu mmoja alisema kuwa hata lile bomu la 911, lilipangwa, kitaalamu, na mlengwa alishagundulikana,swali ni nani...

Tuyaache hayo maana ni mjadala mrefu, kwani sasa hivi dunia imegubikwa na mjadala mwingine wa friimasoni....akili zinayumbishwa,na sijui ni nani huyo tena, ipo siku iatgundulikana, lkn lengo litakwua limetimia.

Mkuu, hizi sherehe na mtindo wa kusherehekea ni mipango madhubuti iliyopangwa kinamna, yale yale. Na nikikumbuka vity vyako, vya naman ya kipekee kuhusu `mambo ya mwanadamu ya kinyume nyume, badala ya kushereheka sikukuu ya uhuru, tunajikuta tunamtukuza huyo huyo alitupa huo uhuru.

Hivi hatujui kuwa hata hii miezi ya mwaka, ni miungu ya wapagani...mbona kila siku tunalaaani kuabudu mizimu, tunalaani kuabudu mashetani tunalaani mengi,lakini kila siku tunaabudu miungu ya wenzetu, hebu tujiulize, kwanini....

Hiyo ni kazi ya ubongo, wenzetu wana makadirio, ya miaka kenda mbele, na kila walilokadiria wanajua tutafanya nini, na ili iweje kwao, ....huo ni nini kama sio `ukoloni mamboleo....'

Mimi mkuu sijui maana nikiwaza sana, nitajikuta natunga kisa kingine hapa kwako. Nisamehe mkuu,ni hayo ....

Mkuu tupo pamoja, kama nimekosea reekbisha!