Kwanza sikiliza UKARIBISHO WA Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar.
Tarehe: SEPTEMBA 15, 2012
Kiingilio: BURE
Muda: (Saa 4:00 asubuhi – Saa 12 Jioni)
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Washington D.C. unawakaribisha Watanzania wote waishio maeneo ya DMV (District of Columbia, Maryland na Virginia) na vitongoji vyake, kuhudhuria siku ya Mtanzania, ambapo waTanzania watashiriki kuonyesha bidhaa, tamaduni, mila na desturi za Kitanzania kwa wageni (waMarekani na wa mataifa mengine) watakaotembelea ubalozini.
Madhumuni makuu ya Ubalozi kuandaa Siku ya Mtanzania
Kwanza ni kuwaelimisha wenyeji wa Marekani kuhusu Tanzania.
Pili kuitangaza zaidi Tanzania kwa kuvutia watalii wengi kutembelea Tanzania.
Tatu ni kutambulisha na kutangaza biashara mbalimbali na huduma zitolewazo na waTanzania waishio hapa Marekani.
Ubalozi unaomba Watanzania wenye bidhaa mbambali za Kitanzania, mapishi (wenye leseni), vikundi vya ngoma, muziki, mitindo, na waTanzania wenye kampuni za utalii, kujiandikisha ubalozini kuanzia tarehe 1 hadi 15 Agosti, 2012 kwa maandalizi ya siku hiyo.
Kwa Watanzania watakaopenda kujitolea kushiriki siku hiyo au kuonyesha bidhaa mbalimbali wajiandikishe kwa wafuatao:
- Dkt. Suitbert Mkama 202 884 1087 au smkama@tanzaniaembassy-us.org
- Asia Dachi 202 884 1096 au adachi@tanzaniaembassy-us.org
- Rosemary Mziray 202 884 1081 au rmziray@tanzaniaembassy-us.org
Ubalozi unapenda kuwahamasisha Watanzania kuvaa vazi la Kitanzania.
Karibuni Wote
IFUATAYO NI RATIBA YA MATUKIO YA LEO
1 comment:
nimependa sana mnavyowasiliana mkiwa huko ughaibuni....watanzania tumeumbwa na upendo....wenye tija...pamoja na nguzo isiyoteguka.shadrack john msuya from mwanza tanzania
Post a Comment