Monday, October 8, 2012

Maendeleo ya msiba Washington DC

Watanzania wenzangu DMV tumepatwa na msiba kama mlivyosikia kwenye vyombo vyetu vya habari siku ya Ijumaa October 5 Dada yetu, Mtanzania mwenzetu Clarrise Maya Niyonkuru aliaga Dunia.
Marehemu Clarrise kuna wakati alilazwa Washington Hospital Center na tukajaribu kutafuta ndugu zake kupitia mitandao mbambali.

Watanzania wenzangu huyu ni Mtanzania mwenzetu, na anastahili kuzikwa kama Mtanzania yeyote na hana ndugu anaowategemea zaidi yetu Watanzania tuishio Marekani hususani DMV.

Tunaomba ushirikiano wako, chochote kile ulichokua nacho kitasaidia na hatimae kuwezesha mazishi ya Clarrise Maya Niyonkuru. Kwa Wakaazi wa DMV tunaombwa tufike nyumbani kwa marehemu ambako msiba upo na kuna kitabu cha rambirambi address ni
6731 New Hampshire Ave, Apt 613,
Takoma Park, MD 20912
Au unaweza kuchangia kupitia Citi Bank Jina la A/c Z-Atlantic acc # 4971703057 Route # 021000089

Tunategemea kumzika marehemu hapa DMV tarehe bado hatujajua lakini mtataarifiwa na vyombo vyetu vya habari mara tutakapopata michango ya kutosha. jukumu hili ni letu sote ushirikiano wetu na umoja wetu bila kujali itikadi zetu kwa pamoja tunaweza.

Leo Jumatatu October 8, 2012 saa 11 jioni kutakua na harambee nyumbani kwa marehemu ya kujaribu kupata pesa zitakazowezesha mazishi ya mpendwa Dada yetu, Rafiki yetu na Mtanzania mwenzetu gharama za funeral home na mazishi ni $7,500 Tunaomba ushirikiano wako, kutoa ni moyo leo kwa Clarrise kesho ni mimi na wewe.

Kwa mawasiliano zaidi na maelekezo tafadhali piga simu
Ellis Kibwere 202 306 5252
Perpetua Nyagerera 302 404 7695
Mayor Mlima 301 806 8467
Asia Rashidi 301 537 9748

Asante.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

poleni sana kwa msiba!!

emuthree said...

Poleni sana, kwa kupotelewa na mpendwa wetu huyo,twamuomba mungu ailaze roho yake mahala pema peponi

Mija Shija Sayi said...

Poleni sana kwa msiba..