Wednesday, October 10, 2012

Maendeleo ya msiba Washington DC

Maendeleo ya msiba wa Dada yetu, mpendwa wetu na Mtanzania mwenzetu, Clarrise Maya Niyonkuru mpaka sasa michango iliyokusanywa ni:
Cash $1,630
Checks $300
Jumla ni 1,930
Pesa inayotakiwa Funeral Home na mazishi ni 7,500 kiasi kilichobaki ni 5,570
. Watanzania wenzangu huyu ni Mtanzania mwenzetu, na anastahili kuzikwa kama Mtanzania yeyote na hana ndugu anaowategemea zaidi yetu Watanzania tuishio Marekani hususani DMV.
Tunaomba ushirikiano wako, chochote kile ulichokua nacho kitasaidia na hatimae kuwezesha mazishi ya Clarrise Maya Niyonkuru. Kwa Wakaazi wa DMV tunaombwa tufike nyumbani kwa marehemu ambako msiba upo na kuna kitabu cha rambirambi address ni
6731 New Hampshire Ave, Apt 613,
Takoma Park, MD 20912
Kuna mabadiliko ya A/c ya Bank sasa tumia hii Citi Bank Jina la A/c Mayor A. Mlima acc # 678528767 Route # 254070116
Add ya Bank ni:
7633 New Hampshire Avenue,
Langley Park, MD 20903
Tunategemea kumzika marehemu hapa DMV tarehe bado hatujajua lakini mtataarifiwa na vyombo vyetu vya habari mara tutakapopata michango ya kutosha. jukumu hili ni letu sote ushirikiano wetu na umoja wetu bila kujali itikadi zetu kwa pamoja tunaweza.
Tafadhali tujitahidi kufika nyumbani kwa marehemu mida ya jioni kuanzia saa 12 kama unachochote tafadhali tunaomba tukampumzishe mpendwa wetu, Dada yetu, Mtanzania mwenzetu, ameteseka sana na ugonjwa, Tafadhali mpunguzie mateso ya baridi anayopata funeral home, chochote kile ulichonacho kitasaidia na hatimae kuwezesha kumpumzisha mpendwa wetu Clarrise Maya Niyonkuru katika nyumba yake ya milele.
Tunaomba ushirikiano wako.
Kwa mawasiliano zaidi na maelekezo tafadhali piga simu
Ellis Kibwere 202 306 5252
Perpetua Nyagerera 302 404 7695
Mayor Mlima 301 806 8467
Asia Rashidi 301 537 9748
Asanteni

1 comment:

emuthree said...

Kweli kutoa ni moyo, tusichangie harusi tu na masherehe,hapo ndio sehemu muhimu ya kuchangia