Wednesday, December 19, 2012

Buriani Dada-Rafiki Amina Singo

Ni saa kumi alfajiri ya jumapili (Desemba 16, 2012). Alarm inasikika nami naamka kuinyamazisha.
Kwa kuwa alarm hiyo ipo kwenye simu hivyo naamua kufungua kuangalia kama kuna ujumbe wowote ama simu iliyokuja wakati nimelala kwa kuwa mara zote nilalapo huwa naondoa mlio kuepusha kuamshwa na simu usiku.
Na kweli. Kuna simu mbili zilizopigwa na Kaka Ally Kashushu toka Dar lakini kwa kuwa sikupokea, kaamua kuniachia ujumbe wa maandishi. Mfupi sana wenye maneno dazeni usemao..."HABARI ZA LEO? NAKUJULISHA KUWA DADA YETU MPENDWA AMINA SINGO AMEFARIKI DUNIA"
Amina Singo a.k.a Mwasi kitoko a.k.a champione d'Afrique alipokuwa akiungurumisha muziki wa kiAfrika ndani ya Times FM
Dah!!!!
Namshukuru Kakangu Kashushu kwa taarifa.
Sitaki kusema kuwa sitaki kuamini, lakini ukweli ni kuwa nasikitika mno.
Amina. Dada tuliyeunguruma wote kwenye SPORTS na kisha kipindi HIKI CHA SUNRISE YA 100.5 TIMES FM (2001-2003)

Amina....
Dada ambaye kwa "kusota" naye, nilikuwa jasiri zaidi sasa hayupo nasi tena.
Si muamini sana wa KULIA kitokeapo kifo, bali huamini katika KUMSHUKURU MUNGU KWA MAISHA YA MPENDWA NIMPENDAYE, lakini hapa naona chozi likidondoka.
L-R: Amina Singo, Deus Saleh, Jamillah Kilahama, Mmmmmh!, Sister V, Sultan Sikilo.
Those happy days (actually my last day) at Times Fm
Historia ya maisha yako (ambayo ulishirikiana nami) na harakati za kusaka maisha kwako mpaka ulipofikia vilinifanya nisikate tamaa.
ULINIPA TUMAINI
Najua unajua nilikuthamini kiasi gani, na unatambua mchango wako katika ukuaji wangu kikazi.
Mara ya mwisho tulipochat nilianza kwa swali kuwa "Haya Mama Aggie. Nijuze maendeleo" nawe ukanijibu kuwa "Namshukuru Mungu Bandio ameniinua nimepona na natarajia kijiunga Tumaini University pia nimeamua kumpokea Bwana.....nimebadili dini pia mwaya! najiona ni mwenye Amani sana kwa sasa"
Mpokigwa Fred, Mimi, Amina Singo na Deus Saleh
Niliuchukulia huu kama UAMUZI WAKO KUJIANDAA KI-IMANI.
Nami nikakueleza kuwa "Lolote jema ufanyalo, NAKUTAKIA NA KUKUOMBEA MAFANIKIO"
AMINA...
Hakuna maneno ninayoweza kusema ambayo yatawiana na namna nilivyothamini mchango wako maishani mwangu.
NAMSHUKURU MUNGU KWA MAISHA YAKO.
KWA NAFASI NILIYOPATA KUFANYA KAZI NAWE.
KWA MAWAZO TULIYOBADILISHANA.
KWA NILIYOJIFUNZA KWAKO
Na sasa naamini kuwa umepumzika mahala palipo na amani.
NTAKUKUMBUKA MAISHA YANGU YOTE...KWANI WEWE NI KATI YA WACHACHE TULIOSHIRIKIANA SANA WAKATI WA KUANZA FANI hii ambayo wengi wao walituona kama tunaopoteza muda na hatungeweza kufanikiwa.
Kila mmoja katika kundi letu alifanikiwa na anajitegema huko alipo. NA ULILIONA NA KULISEMA HILI.
Sina cha kulia tena kuhusu maisha yako.
Nasherehekea kuwa uliishi nasi na tulijifunza kitu toka kwako
I know you'll live again

REST IN PEACE Dada Amina.

No comments: