Sunday, January 13, 2013

Ana kwa Ana ya Lokassa ya Mbongo na Vijimambo (II)

Hivi karibuni, blogger mwenzetu Luke Joe wa VIJIMAMBO alifanya mahojiano na
mkongwe wa ucharazaji wa gitaa la kati barani Afrika, LOKASSA YA MBONGO katika utaratibu wake mpya wa kuhojiana wadau mbalimbali.
Leo Jumatatu January 14, 2013 anawaletea sehemu ya pili ya mahojiano haya ambapo Lokassa anaeleza jina alilopewa na Tabu Ley Rochereau wakati akiwa na miaka 16.
Katika sehemu hii pia, Lokassa ataelezea mkasa uliomkuta yeye na wanamuziki wengine wanne baada ya kumkibia Tabu Ley na kujiunga na Sam Mangwana na jinsi gani walivyotaabika nchini Ivory Coast kwa kushinda pwani na usiku kulala sokoni
Je anatoa ushauri gani kwa wanamuziki wanaochipukia, Je katika zile nyimbo za Tanzania alizopiga vipande vipande zilizojulikana kama "NAIROBI NIGHT", pesa ya kuzitumia zile nyimbo alilipwa nani ? Tabu Ley na Sam Mangwana wapo wapi sasa hizi,pamoja na mambo mengine mengi UNGANA NAO

No comments: