Sunday, February 24, 2013

Thaminisha.....ABOU SHATRY

Zaidi ya umdhaniavyo..
Mpishi wa mengi asiyepokea "tip" halali kwa kazi zake

Wengi wetu tumekuwa "walaji" wa migahawani / ama tumeshuhudia baadhi ya taratibu za walao migahawani ambapo wahudumu (Waiters / Waitresses) wamekuwa wakipokea "tips" kutokana na huduma nzuri itolewayo mahala hapo.
Na ukweli usiopingika ni kuwa, haijalishi mhudumu ametabasamu kwa kiasi gani, ama ameleta huduma kwa kiasi gani, ama amewapa meza muitakayo ama lolote linaloongeza uwezekano wa "tips" hizo, ukweli wa mambo utabaki kuwa NI LAZIMA CHAKULA MLACHO KIWE KIZURI ILI "TIP" HIYO ITOKE.
Nimeanza na mfano huu kwa kuwa naamini kuwa WAPISHI WENGI (ambao ndio chanzo halisi cha tips hizo) huwa hawaonekani na pengine hawathaminiki katika utoaji wa TIPS hizo.
Nazungumzia TIP kama kiwakilishi cha SHUKRANI na / ama SIFA ambazo watu hupata / kunyimwa kulingana na kile wafanyacho.
Na hili ni (kama vile) jambo la kawaida kwa jamii.
Kuwa na NYOTA WACHACHE japokuwa tunajua fika kuwa kazi iliyofanyika imehusisha wengi, na wakati mwingine wale walioonekana ndio waliofanya kazi zaidi.
Kwani nikikuuliza kuhusu UHURU WA TANZANIA, unajiwa na jina ama majina mangapi?
Lakini unaamini hao uwatajao ama kuwawaza ndio PEKEE waliowezesha UHURU WA TANZANIA?
La hasha..
Nikirejea kwa Kaka-Rafiki Abou Shatry, wengi hawatambui THAMANI YAKE kwa kile waonacho humu na kwingine.
Mbali ya kuwa ni bloga mahiri kupitia blog yake hii ya SWAHILIVILLA lakini pia...
Abou ni zaidi ya blogger mwenzangu.
Ni zaidi ya mshirika katika kazi. 
Zaidi ya Rafiki yangu
Zaidi ya Kaka yangu na zaidi ya mTanzania mwenzangu.
 Amekuwa mtu ambaye katika "level" ya kifamilia, tumeungana zaidi ya maelezo.
Katika "level" ya kazi, tumejuana na kushirikiana zaidi ya maelezo.
Abou amekuwa MPIGAPICHA NA MHARIRI MKUU katika takriban Video zote hizi za Jamii Production na ameshiriki katika utayarishaji mzima wa mchakato wa mahojiano.
Pamoja na "credits" zitokazo mwisho wa mahojiano bado inakuwa ngumu kwa watu kutambua THAMANI ya kazi na zaidi KIPAJI CHA UBUNIFU alichobarikiwa nacho Kaka Abou.
Niweke wazi kuwa, licha ya kupokea pongezi nyingi kwa kazi zetu, lakini MCHAKARIKAJI MKUU wa kusaka, kutekeleza na hata kuboresha kazi za USHIRIKA WETU ni Kaka Abou.
Iwe ni kutengeneza banners (kama hiyo ya Jamii Production  hapa chini ambayo bado naamini kuwa NI "NYEPESI" LAKINI YENYE KILA UZITO UNAOSTAHILI) ama iwe ni kuhariri na kurekebisha na kusambaza video za mahojiano, Abou amekuwa mstari wa mbele katika kuboresha hilo.
"Mkono" wa Abou ndani ya dakika chache za kupata wazo.
Umakini wa kazi yake, umeifanya jamii (inayoangalia videos zetu) kunufaika na kila kitendekacho.
NI MKALI KARIKA KAZI na KILICHO BORA NDILO LENGO LAKE, na mara zote anajua namna muafaka ya kukisaka.
Abou ndiye mkosoaji namba moja wa kazi zetu (weka mbali "better halves" wetu) hivyo kuepuka "lawama" zake ndiyo chachu ya maandalizi zaidi katika mahojiano.
Lakini...
Abou ni zaidi ya mwana Jamii Production.
Ni Mume, ni Baba, ni Mwanajamii na zaidi ya yote muumini mzuri ambaye kwa maisha aishiyo amekuwa mfano kwa wengi.
Ushirikiano wake katika jumuiya mbalimbali hapa DMV umemfanya awe mfano kwa wengi.
Binafsi namchukulia kama nilivyosema hapo awali......
Abou ni zaidi ya blogger mwenzangu.
Ni zaidi ya mshirika katika kazi.
Zaidi ya Rafiki yangu.
Zaidi ya Kaka yangu na zaidi ya mTanzania mwenzangu.

KATIKA KILA UFURAHIALO KWENYE VIDEO ZA JAMII PRODUCTION, TAMBUA KUWA YUPO "MPISHI" AMBAYE MARA NYINGI HAONEKANI.
Naye ni Abou...AMBAYE LEO NAMTHAMINISHA KWA YOTE MEMA ATENDAYO KWENYE JAMII YETU.

Heshima kwako Kaka Abou..Utendalo ni HAZINA KWA JAMII YETU 


**THAMINISHA ni kipengele kinachounganisha makala ama matoleo mbalimbali ya watu mbalimbali wanaojitolea kuboresha maisha ya wengine na hata wale wanaoona vema kuthaminisha yale waliyotendewa na wengine. Kwa matoleo zaidi BOFYA HAPA**

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli ni kweli kabisa mtendalo ni hazina kwa jamii..kila la kheri