Thursday, March 7, 2013

Kwenu WANAWAKE WOTE DUNIANI....HERI KWENU

Tribute to the Women of the World
This is a humble sampling in tribute to some of the great women throughout history ... set to the song, Hero, by Mariah Carey.


Kila mwaka wanawake na walimwengu kote ulimwenguni huadhimisha SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE DUNIANI ambayo husherehekewa tarehe 8 Machi.
Mamia ya shughuli na matukio hufanyika ndani ya mwezi mzima wa Machi kusherehekea na kuadhimisha harakati za wanawake duniani katika Uchumi, Siasa na ukombozi wa Jamii ambapo Serikali, Vikundi vya wanawake na mashirika mbalimbali huchagua kauli mbiu kuakisi masuala ya kijinsia katika jamii husika na ulimwengu kwa ujumla.
Kauli mbiu ya mwaka huu kutoka Umoja wa Mataifa ni AHADI NI AHADI: MUDA WA KUMALIZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NI SASA
Kwa mujibu wa UMOJA WA MATAIFA,
  • manyanyaso ya kijinsia yanayofikia asilimia hamsini hufanywa kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 16.
  • Duniani kote, zaidi ya wanawake milioni 603 wanaishi kwenye nchi ambazo manyanyaso ya kifamilia hayahesabiki kama kosa
  • Wanawake wafikiao asilimia 70 duniani kote wanaarifu kupitia manyanyaso ya kijinsia na ama ya kimwili katika wakati fulani wa maisha yao
  • Zaidi ya wasichana milioni 60 duniani wameolewa wakiwa na umri chini ya miaka 18
Katika kuadhimisha hili, NAUNGANA NA WANAWAKE, WASICHANA NA WALIMWENGU WOTE KATIKA KUKOMESHA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA.
Naungana na Lucky Dube pia katika kuwaombea wanawake kwa MUNGU. Nawaacha na kibao chake GOD BLESS THE WOMEN ambacho mashairi yake yako hapo chini. Sikia anavyowaombea na kuwashukuru. Akiwaita HEROES
HESHIMA KWENU KINAMAMA NYOTE

In the middle of the night I heard her pray so bitterly and so softly yeah...
She prayed for her children
She prayed for their education,
Then she prayed for the man that left her with her children.
We, praise heroes everyday
But there are those that we forget To praise
The women of this world.
They do not run from anything
They stand and fight for what's right
They do not run from anything
They stand and fight for what's right


Chorus
Oh oh oh...
God bless the women

Even when times are so hard
They are so cool, calm and collected.
They do not run from anything,
They stand and fight for what is right
They do not run from responsibilities
They stand and fight for what Is right

Chorus till fade...


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa bila kutusahau wanawake kheri nanyi pia akina baba maana bila ninyi tusingekuwepo..ijumaaa njema kwako pia...

emuthree said...

Mungu wabariki wanawake, wabariki akina mama zetu, kwani wanastahili baraka hizo.