Sunday, April 21, 2013

Wana-Diaspora....Tuwafunze watoto wetu Kiswahili

Hivi karibuni, Jumuiya ya waTanzania hapa DMV imeanzisha madarasa ya kiSwahili kwa watoto.
Mkakati huo ni muenedelezo wa kusaidia kukuza lugha kwa watoto waliozaliwa ama kukulia huku.

Katika hili, mwanaharakati Abou Shatry wa SWAHILIVILLA BLOG alianza kuandaa madarasa kwa njia ya video ili kuwezesha kuelewa kwa urahisi.
Hapa, ameanza kwa kutengeneza video ya majaribio inayoonyesha baadhi ya Wanyama na Ndege na anakaribisha maoni ya namna ya kuboresha mkakati huu.

Ni jambo jema na la kujivunia kuona idadi kubwa ya watoto wakihudhuria madarasa haya, jambo linaloonyesha mwamko wa wazazi kuwafunza watoto lugha yao ya asili Madarasa haya yamegawanywa katika makundi kulingana na mahitaji ya watoto na yanaendelea kila Jumamosi

Baadhi ya watoto waliohudhuria darasa hili la watoto la kiswahili kama walivyonaswa na kamera ya Blogu ya Vijimambo

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Nimependezwa sana na taarifa hii..pia nimeona wivu kiduchu kwa vile nimekuwa nikifanya utafiti huo hapa ili wanetu wapata lugha tya kiswahili shuleni ,,lakini haiwezekana ni wachache..HONGERENI