Saturday, April 20, 2013

Ana kwa Ana na Mhe. Leticia Nyerere


Karibu katika mahojiano kati ya Jamii Production na Mbunge wa Viti Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Leticia Nyerere.
Yeye ni Mjumbe wa kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Katika mahojiano haya yaliyofanyika Machi 15, 2013, Mhe. Nyerere amezungumzia mambo mengi ikiwemo
1: Historia ya maisha yake
2: Wajibu wa mbunge wa viti maalum
3: Ushirikiano wa wabunge wanawake katika kumkomboa mwanamke
4: Utata wa uraia wa nchi mbili
Pia mtazamo wake katika Mchakato wa katiba mpya, uongozi wa majimbo Tanzania, kutenganisha chaguzi za Rais na Wabunge, kuwa na mabunge mawili nchini, mchakato wa kuwapata wabunge wa viti maalum, na mengine mengi
Karibu uungane nasi

1 comment:

Mija Shija Sayi said...

Hii ni mara ya kwanza kumsikia Dada Leticia akiongea, kwa ufupi nimemkubali!

Mambo yoote aliyoyaongea nimeyakubali kabisa, lakini hili la kubadili mfumo wa Elimu, nimelikubali na kulikamata na nitaanza kulipigia kelele.

Tanzania mfumo wa elimu tulio nao ni wa kukaribisha umasiki na ujinga. Tunakazania kufaulu mitihani ili iweje? Mbaya zaidi hatuchunguzi hata kufaulu kwenyewe ni kwa kukariri au kuangalizia !!

Kama alivyosema Da' Leticia, mfumo ubadilike na tulenge kumjenga mtoto kuja kupambana na maisha sio kupata mia kwa mia halafu hana skills za kuleta mabadiliko duniani!

Bado narudia na kurudia kumsiliza ili nihakikishe vinaniingia vizuri kichwani!

Asante kaka Bandio kwa kutuletea mahojiano haya.