Monday, May 6, 2013

Ya Ruge na Jay Dee.....Bongo Flava kama uSHOGA

ONYO....Habari ni zaidi ya kichwa chake. Japo lazima iendane nacho
Hivi karibuni kumetokea (kile kinachoonekana kama) ugomvi kati ya mmoja wa wadau wakubwa katika muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni kiongozi mwandamizi wa Radio Clouds Bwn Ruge Mutahaba na nyota wa muziki nchini Bi Judith Wambura (Lady Jay Dee). 
Ugomvi ama kutoelewana huku kumekuwa dhahiri kwa jamii baada ya mfululizo wa matam,shi ya Lady Jay Dee kuhusu kituo cha Clouds na hata Bwn. Ruge na Bwn. Joseph Kusaga (mmiliki wa Clouds Media Group).
Na mambo yakazidi kuwa wazi zaidi baada ya Lady Jay Dee kuandika WOSIA WAKE iwapo atatangulia kabla ya Ruge na Kusaga (usome HAPA) Baada ya hapo, Bwn Ruge aliamua kuelezea suala hili pamoja na mengine mengi kwenye kipindi cha Power Breakfast ambacho kilirekodiwa na maelezo yake kuwekwa HAPA Pamoja na kusoma na kusikiliza pande zote za mgogoro huu ambao naamini haustahili kuwepo, bado naona KUNA JAMBO LA KUJIFUNZA.
Kuna ukweli juu ya kile kizungumzwacho na wote na kuna haja ya kuona WAHUSIKA WANASHUGHULIKIA HILI.
Kama alivyosema Bwn. Ruge, kuna haja ya wahusika kushughulikia yale yanayoendelea huko mitandaoni, na nakubaliana naye, kama ambavyo naona uhitaji wa mamlaka husika kufuatilia malalamiko ya Lady Jay Dee ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu.
Ukweli ni kuwa MAMLAKA HUSIKA HAZIFANYI KAZI ZAKE. Kama nilivyopata kuandika mwaka jana kuhusu KISWAHILI KAMA USHOGA (rejea hapa), naona ndilo linaloendelea hapa, ambapo mmomonyoko wa maadili katika ngazi zote za biashara ya muziki nchini Tanzania unaachwa bila kushughulikiwa katika hatua hizi za awali mpaka pale watakapoanza kushikiana mtutu ndipo tujiulize wameanza lini?
Panafuka moshi hapa, na hakika KUNA MOTO CHINI ambao ni lazima tutambue kuwa tukiuacha unaweza kuendelea kuleta madhara.
CHANGAMOTO YETU ni.....
TUSIACHE HAYA YANAYOENDELEA KUFUKUTA YAFIKE MBALI ZAIDI kama tulivyofanya kwenye ushoga 
TUSIACHE mpaka wengine ambao hawajawa na dhamira halisi ya kujiunga na ugomvi huu wafanye hivyo (kama tulivyofanya kwenye ushoga)  
TUSIPUUZE KILIO CHA LADY JAY DEE WALA MAELEZO YA RUGE MUTAHABA.
Kuna ukweli katika yaliyosemwa na pande zote na hakuna haja ya kuacha hili nalo likafikia mahala ambapo walio nje watatulazimisha kulishughulikia.
Tumepuuza mengi na athari zake tumeziona.
KUNA LA KUJIFUNZA katika hili. Na wakati wa kulishughulikia ni sasa. Wote wanaohusika na hili wameonyesha nia ya kulishughulikia, kulimaliza na kuendelea na maisha yao kama kawaida.
Alipohojiwa HAPA na Kaka Sunday Shomari , Lady Jay Dee amenukuliwa akisema “Wasiponifuatilia ntanyamaza watakuwa marafiki zangu tutapatana” na wakati huohuo, Ruge amesema wakikubaliana, watatafuta sehemu "neutral" na kujadili hili.
NIA IPO, UWEZO UPO...SASA LILILOBAKI NI KUTEKELEZA kazi hiyo.
Tusiliache hili likafika lilipofika la ushoga kisha tukasema hatuna namna ya kufanya. TUNAYO SASA.

Na huu ni mtazamo wangu kwa namna nionavyo tatizo....
Labda NAMNA NIONAVYO TATIZO NDIO TATIZO

No comments: