Tuesday, September 25, 2012

KISWAHILI kama USHOGA.......na watendakazi wetu "wafu"

Photo Credits: Mugishagwe Bolg
Februari 24, 2010 niliandika POST HII iliyokuwa na kichwa kisomekacho Wanasiasa wetu na sakata la Ushoga / Usagaji. kuhusu pendekezo la Mbunge wa Uganda kuwa watu wanaoendekeza vitendo vya ushoga wauawe.
Nilipinga nikianza na maelezo SAHIHI kuwa mimi si shabiki wala siendekezi wala kuunga mkono ushoga, lakini sikuamini kama ilikuwa sahihi kuanza kuwaua sasa ilhali hatukuona jitihada makusudi kuwasaidia wasiwe walivyo.
Katika tileo hilo, niliandika
"Tuanze kwa kutambua kuwa MASHOGA NA WASAGAJI ni wenzetu, waliozaliwa katika familia ambazo nyingi ni za watu wasio mashoga wala wasagaji.
Kwa hiyo kama wamezaliwa katika familia zilizo tofauti na walivyo leo, NI LAZIMA TUJIULIZE kuwa NI WAPI TULIPOJITENGA NAO NA KUWAFANYA / KUWAACHA WABADILIKE NA KUWA WALIVYO?
Sisi kama JAMII TUNA SEHEMU YA LAWAMA kwa kuwa ama hatuwasaidii kutokuwa walivyo, au tunachochea kuwa walivyo hata kama twatenda haya bila sisi kujua. Suala hili la USHOGA NA USAGAJI halijaanza leo wala mwaka jana ambapo wanasiasa wameonekana kulivalia njuga.
Nakumbuka nikiwa mdogo tulisikia utani wa "kushikishwa ukuta huko Lamu" na baada ya kukua na kung'amua nikajua kuwa ni suala la USHOGA NA USAGAJI lakini hakuna aliyethubutu kujadili nasi kuhusu suala hilo mpaka leo hii ambapo mambo yanaonekana kuwazidi nguvu naanza kuwaona WANASIASA wakija na hatua zao za zimamoto ambazo zinafikia hatua ya kuwaadhibu hata wale watakaoshindwa kuwataja mashoga na wasagaji wawaju.
TATIZO KUBWA NI MOJA KWA NCHI ZETU ZA KIAFRIKA.
Hakuna kiongozi anayetaka kujishughulisha na chanzo cha tatizo. Wanakurupuka kwa namna za KUAHIRISHA tatizo na kisha kutumia uhahirisho huo kujipatia kura za kurejea madarakani.
Kisha tatizo larejea.
Wakati nasikia habari za kile nilichokuja kung'amua kama matendo ya kishoga na usagaji nilikuwa mdogo, na nina imani kuwa walikuwepo mashoga na wasagaji wachache saana ukilinganisha na sasa lakini kile wanachokiita "mila za kiAfrika" ziliwazuia wazazi, walezi na viongozi kujadili ATHARI za kujikita kwenye tabia mbaya kama hizo na matokeo yake ndio tuonayo sasa ambapo tatizo hili LIMEOTA MIZIZI na twasikia harakati za KUWAFUNGA NA KUWAUA.
Kisha baada ya hapo?????"
SASA TUHAMIE KWENYE MSHABIHIANO WA USHOGA NA KISWAHILI.
Ni nani asiyejua namna ambavyo kiswahili kinaharibiwa hivi sasa?
Yaani tangu kuingia kwa hivi viwezeshaji vya mawasiliano vilivyo na kiwango cha maneno ya kutumia, watu wameanza kuandika lugha ambayo inatupeleka pabaya.
Sijasikia wala kusoma onyo ama maelezo kutoka kwenye vyombo husika katika lugha ya kiSwahili.
Na tunatakiwa kuwaza iwapo hawa watoto (pamoja na wageni) ambao wameanza kujifunza kiSwahili katika zama hizi za Twitter na Facebook na Text msgs watakuja kujua kiSwahili halisi.
Hawa WATAWALA wenye mamlaka na ambao wanajua kuwa kile kizungumzwacho na "vijana wa kisasa sio kiSwahili sahihi" wanafurahia na kuangalia "ubunifu na utundu" wa WAHARIBIFU HAWA na kushindwa kusema lolote.
Wako wapi BAKITA ambalo liliundwa chini ya sheria namba 27 ya Bunge ya mwaka 1967.
Na ni nini kazi yao?
Kwa mujibu wa MAELEZO KATIKA TOVUTI YAO HII, wanasema "Kimsingi, BAKITA ndiyo inayofanya kazi ya kuratibu na kusimamia shughuli zote za kukuza, kuendeleza na kueneza Kiswahili nchini."
Katika tovuti hiyohiyo, BAKITA wanasema kuwa DHAMIRA YAO ni "Kukuza, kustawisha na kuhimiza matumizi ya Kiswahili fasaha ndani na nje ya nchi kwa ushirikiano na wadau wengine." na pia DIRA YAO ni "..kuwa taasisi yenye nguvu kisheria, kifedha na inayotambulika kitaifa na kimataifa katika kuratibu, kusimamia na kukuza maendeleo ya lugha ya kiswahili. Kukubalika kwa matumizi ya Kiswahili katika Umoja wa Afrika (UA) na mafanikio ambayo lugha hii inayapata, vinatupa tumaini na imani kwamba kile tunachokiamini na ambacho tumekuwa tunakiamini siku zote kuwa Kiswahili kitakubalika duniani kote sasa taratibu kinaelekea kuwa kweli na kwa hakika zaidi."
WAKO WAPI?
WANAKABILIANA VIPI NA HILI LINALOONGEZEKA KILA SIKU?
Ukweli ni kuwa vijana wengi wanaharibikiwa kwenye mitandao ambayo BAKITA haina mpango nayo.
Tukishindwa kuzuia sasa mmomonyoko huu, tutakuja kukurupuka na kutoa kauli kama zilizotokea kwenye suala la ushoga.
Katika hili la mashoga, niliwaomba watawala, kuwa Chonde chonde "waheshimiwa". Kabla hamjasema tena ya Cameron....... na humo nikawakumbusha kuwa "Kama suala la mashoga na wasagaji linawakera kama ambavyo mmeonyesha kwenye kauli zenu, ni yapi ambayo mmeyafanya kulipunguza ama kuliondoa? Mimi na ninyi na wasomaji wangu tunajua kuwa kama tungekuwa na mashoga sifuri, basi tusingehofu kuhusu hili.
Lakini kwa kuwa idadi yao ni kubwa NA INAONGEZEKA KWA UHURU KILA UCHAO, mnaona athari zake. Lakini kabla hamjasema tena juu ya kauli ya Cameron, mtusaidie kutueleza ni yapi mmefanya kupunguza ama kuondoa ushoga Tanzania? Tena nimesikia Mhe Membe akisema SHERIA INASEMA WANAWEZA KUFUNGWA MPAKA MIAKA 30 JELA. Sina hakika ni wangapi walikuwa wakilijua hili, na sina hakika takwimu za Waziri na Rais zaonyesha ni wangapi wameshafungwa kwa hili?"
Sasasaaaa........
Juhudi za haraka na madhubuti zinahitajika kuhakikisha kuwa lugha ya kiSwahili haifikii mahala ambapo hatutaweza kuirejesha inapostahili kuwa.
SERIKALI INASTAHILI KUCHUKUA HATUA, KUHAKIKISHA KUWA INATUNZA LUGHA SANIFU YA KISWAHILI KWA KUWEKA MASHARTI MAKALI KUHAKIKISHA KUWA VYOMBO VYA HABARI  (VILIVYOJISAJILI) VINATUMIA LUGHA SAHIHI NA SANIFU. 

Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA

Tuonane "Next Ijayo"

1 comment:

emuthree said...

Tatizo kubwa labda niseme kuwa Kiswahili hakithaminiwi, labda siku wazungu wakiamua kikiweka kwenye hadhi ya kimataifa.

Kuna mtu aliniambia itafika muda hata baadhi ya maneno ya kiswahili yatakuwa hayatambuliki tena, na kwa vile wenzetu ni wajanja watakuwa wameshayahifadhi,kwahiyo tukiyahitaji itabidi twende kwao kuwapigia magoti.

Mtu ukiacha utamaduni wako wewe ni mtumwa tu, kiswahili ni moja ya utamduni wetu,ndicho kinachotuunganisha kitaifa, kiswahili ndio Tanzania. Sasa tujiulize Tanzania ina nafasi gani katika hii dunia?

Ndio maana hata wakubwa wakienda huko majuu, hawawezi kuongea Kiswahili, wataongeaje Kiswahili?

Kwahiyo hata watu wakiboronga, na kuongea ndivyo sivyo, wakaweka maneno ya bandia ilimradii kionekane kama `kizungu' hakuna shida .

Huoni hata wenyewe wakiongea hawaongea ile lafudhi ya kiswahili, lazima ubane pua kama mzungu. UTUMWA HUO!