Sunday, June 30, 2013

Makamilisho ya Tamasha la Kiswahili ....Masanja, Shilole wawasili DC

Sherehe za miaka mitatu ya blog ya vijimambo itakayoambatana na Tamasha la Utamadunmi wa Kiswahili zinazidi kukamilika ambapo wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole ambao wanatarajiwa kutoa burudani siku hiyo wameshawasili hapa Washington DC.
Mgeni rasmi katika siku hiyo ambaye ni Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi anataraji kuwasili alhamis ya Julai 4.
Zifuatazo ni baadhi ya taswira za kuwasili kwa wasanii hawa hi leo
 Wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la Utamaduni wa Kiswahili, Bwn. Baraka Daudi alipokwenda kuwapokea walipotinga uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
 Dada Asha Riz, mjumbe aliyewawakilisha Tano Ladies kwenye mapokezi hayo akipata picha ya pamoja na wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole mara tu walipowasili uwanja wa ndege wa  kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
Wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole wakielekea kuchukua usafiri kuelekea Washington, DC
 Masanja na Shilole katika picha ya pamoja nje ya uwanja wa ndege waKimataifa wa Dulles.

Picha kwa hisani ya Vijimambo Blog

2 comments:

emuthree said...

Mhh, bahati, iliyoje, `ustar' una manufaa yake, ndio kama hayo. Lakini cha muhimu ni hiyo ajenda, `tamasha la kiswahili' je ni nini kitaweza kukisaidia kiswahili, ili lugha yetu iwe miongoni mwa lugha za kimataifa!

Mzee wa Changamoto said...

Mkuu...ndilo tunalofuatilia na kisha NTAKUJUZA kile kitakachojiri