Karibu katika majaribio ya kipengele cha TUNGO ZETU ndani ya kipindi cha NJE-NDANI kinachotayarishwa na JAMII PRODUCTION Redio kutoka Jiji Washington DC Nchini Marekani.
Katika kipindi cha wiki hii ya Jumapili Aug 18, 2013, tulijaaliwa kuwa na Bwana Yasini Landi pamoja na mkewe Salma Moshi, msanii wa kwanza wa kike kucheza na chatu jukwaani nchini Tanzania.
Mazungumzo katika kipengele hiki yalihusu kuhusu nyimbo za zamani kidogo. Salma alizungumzia wimbo wa DUNIA IMANI IMEKWISHA uliyoimbwa na muimbaji mkongwe Marijani Rajabu, mmoja wa watunzi mahiri wa muziki nchini Tanzania.
Yasin yeye alizungumzia wimbo wa CHATU MKALI uliotungwa na Muhidin Gurumo. Kwa maoni, wasiliana nasi kwa barua pepe jamiiproduction@gmail.com
KARIBU UUNGANE NASI
1 comment:
Mkuu tupo pamoja, naikubali hiyo, natarajia siku moja nitatinga huko, hata kama kwa picha
Post a Comment