Sunday, August 25, 2013

Miaka 50 ya "March On Washington". Mahojiano Na Profesa John Innis Mtembezi

Nilipokutana na Prof John Mtembezi July 22, 2012.
Ni nusu karne sasa tangu kufanyika kwa maandamano makubwa sana ya kudai haki za watu weusi, yaliyofanyika August 28, 1963 katika jiji la Washington hapa nchini Marekani. Maandamano hayo yaliyopewa jina la MARCH ON WASHINGTON,ambayo pia yanakadiriwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya robo milioni, yanakumbukwa na wengi kwa namna nyingi, lakini yamekuwa maarufu zaidi duniani kutokana na HOTUBA iliyotolewa na mwanaharakati Martin Luther King Jr aliyoipa jina la I HAVE A DREAM.
Wiki hii, maelfu ya watu wamekusanyika jijini Washington DC, kufuata pale nyayo zilipokanyaga miaka 50 iliyopita kuelekea katika sehemu ileile yalipohitimishwa maandamano hayo.
Wengi wanaamini kuwa kuna mabadiliko yaliyotokea tangu wakati ule, lakini pia wapo wanaoamini kuwa mpaka sasa, MAPAMBANO dhidi ya ukandamizaji wa haki yapo kama ilivyokuwa wakati ule….japo yawezekana ni kwa namna tofauti kidogo
Kufahamu zaidi, Jamii Production imefanya mahojiano na Prof. John Innis Mtembezi kuhusu miaka 50 tangu kufanyika kwa maandamano hayo
Wakati huo (1963), ndio alikuwa amemaliza High School.
Ameeleza mambo mengi ikiwa ni pamoja na...
Anayokumbuka kuhusu siku hiyo.
Harakati zao (WaMarekani weusi) katika kudai haki zao.
Nini hasa liliwafanya waMarekani weusi waandamane?
Nini kimebadilika?
Nini hakijabadilika?
Kuwa na Rais mweusi, Mwanasheria mkuu mweusi na hata kupata kuwa na Waziri wa Mambo ya Nje mweusi ambaye ni mwanamke ni dalili za ukombozi wa mtu mweusi Marekani?
Kisha akatoa USHAURI WAKE KWA WASIKILIZAJI WOTE POPOTE WALIPO.
KARIBU UUNGANE NASI

No comments: