Thursday, August 22, 2013

MJADALA WA MAONI YA KATIBA MPYA KWA WAKAZI WA DMV


Ndugu watanzania wa Washington DC na vitongoji vyake.
Tunapenda kuwakaribisha katika mjadala wa Katiba mpya ya Tanzania utakaofanyika siku ya Jumamosi (24/8/13) kuanzia saa tisa kamili alasiri mpaka saa kumi na mbili jioni.
Mjadala huu utakaorekodiwa kwenye video utasambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari pamoja na ofisi husika.
WAHUSIKA WANAOTARAJIWA KUSHIRIKI NI:
1: Wawakilishi wa matawi ya vyama vya siasa (CCM, CUF, CHADEMA)
2: Wawakilishi wa Jumuiya na Taasisi za waTanzania 
3: Wananchi wote watakaohudhuria kuchangia na kuuliza maswali.
 Anwani ni
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740


Tafadhali....JIANDAE na Usikose kuhudhuria na kutoa mchango wako ili kufanikisha kupata katiba itakayotufaa sote.KWA UFUPI
Rasimu ya Katiba ina Ibara 240.

MISINGI:
uhuru, haki, udugu na amani

TUNU ZA TAIFA:
Utu,uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi uwajibikaji na lugha ya kiswahili,
-Mgombea Urais umri miaka 40,
-Kiwango cha kura za ushindi za urais ziwe zaidi ya asilimia 50,
-Matokeo ya urais kupingwa mahakamani (surpime cort).

MADARAKA YA RAIS:
-Kubaki kama yalivyo kwenye uteuzi wa viongoz wa ngazi za juu,
-Kushirikiana na taasisi nyingine,na kushauriwa na vyombo vya ulinzi na usalama kuteua nafasi nyingine.

BUNGE,
-Bunge kuwa na madaraka ya kumshitaki Rais,
-Ukomo wa ubunge ni vipindi vitatu,
-wananchi kuwa na uwezo kumuondoa mbunge,
-Spika asiwe mbunge wala kiongoz wa chama cha siasa,

TUME YA UCHAGUZI,
-Kuitwa Tume Huru ya uchaguzi,
-wajumbe kuomba nafasi na kufanyiwa usaili na Kamati ya uteuzi,
-M/kt wa kamati ya uteuzi ni Jaji Mkuu,

MAHAKAMA;
-Kuunda suprime court (itakayosikiliza kesi za matokeo ya Uchaguzi nafasi ya Urais).

MUUNGANO;
Serikali tatu,
Mambo ya muungano yamepungua kutoka 22 hadi 7,

BUNGE LA MUUNGANO;
Mawaziri wasizidi 15,
Wabunge 70!
Hamna mahakama ya kadhi.

DHANA YA RASIMU SIFURI YA MAPENDEKEZO YA WADAU KUHUSU KATIBA MPYA YA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA TANZANIA SURA
Rasimu ina Sura 15, ibara 130 na nyongeza tatu.
Sura ya kwanza inahusu Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania na watu wake. uk. 1-4
Sura ya pili inahusu maadili na misingi mikuu ya taifa. uk. 5-7
Sura ya tatu inahusu haki kuu za binadamu na wajibu muhimu uk.7-21
Sura ya nne inahusu serikali ya shirikisho uk. 22-42
Sura ya tano inahusu Bunge la shirikisho uk. 43-63
Sura ya Sita inahusu mahakama kuu ya shirikisho uk. 64-67
Sura ya Saba inahusu Mahakama ya Rufani ya Shirikisho uk. 68-73
Sura ya nane inahusu vyombo vya dola vya Tanganyika na Zanzibar uk. 74-78
Sura ya Tisa inahusu sekretarieti ya Maadili uk. 79-80
Sura ya kumi inahusu masharti kuhusu fedha za Shirikisho uk. 81-88
Sura ya ya Kumi na moja inahusu madaraka ya umm auk. 88
Sura ya kumi na mbili inahusu majeshi ya ulinzi uk. 89
Sura ya kumi na tatu inahusu mamlaka ya kutunga katiba uk. 90-92
Sura ya Kumi na nne inahusu Tuma mbalimbali za taifa uk. 92-99 na
Sura ya kumi na tano inahusu mengineyo uk. 99-105

NYONGEZA:
Rasimu sifuri ina nyongeza tatu kama ifuatavyo:
(i) Nyongeza kuhusu mambo ya shirikisho
(ii) Nyongeza kuhusu mambo yasiyo ya shirikisho na
(iii) Nyongeza kuhusu idadi ya wizara za shirikisho 1

No comments: