Tuesday, October 1, 2013

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA. Kikao cha Baraza Kuu La Umoja wa Mataifa @Capital Radio

Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kimeanza jumatatu wiki hii  huko New York nchini Marekani huku kikiwa kimetanguliwa na uwezekano wa matukio mengi ya kihistoria kujitokeza katika kikao hiki.
 Rais Jakaya Kikwete alihutubia Baraza hilo siku ya Alhamis na ajenda yake kuu ikiwa ni MAENDELEO BAADA YA MWAKA 2015.
Lakini, mbali na mjadala mgumu kuhusu Syria, bado suala la nchi ya Iran kutuhumiwa kuendelea kurutubisha silaha za nyuklia lilikuwa ni sehemu kubwa ya mazungumzo yaliyokuwa yakitegemewa kuchukua nafsi katika hotuba za kikao hicho
Ifuatayo ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30am) kwa saa za Afrika Mashariki
Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Septemba 28, 2013

Chini ni Hotuba ya Rais Kikwete alipohutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 26, 2012

No comments: