Wednesday, October 16, 2013

E-government, Big Results Now ndio suluhisho la urasimu Tanzania- Serukamba


IMG_4313
Mbunge wa Kigoma mjini na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Bw.Peter Serukamba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya miundo mbinu ya bunge ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania alifanya mahojiano katika studio za idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika hivi karibuni.
Katika mahojiano hayo pamoja na mambo mengine alizungumzia majukumu ya kamati yake pamoja na changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu hayo ikiwa ni pamoja na urasimu, kuwapa nafasi ya wakandarasi wazawa, Millenium Challenge akaunt na mengine mengi.
Akijibu swali kuhusu tatizo la urasimu ameeleza kuwa e-government au serikali mtandao na mpango wa rais Kikwete wa BRN-(Big Results Now) kuwa ndio njia itakayosaidia kutatua tatizo hilo la urasimu ungana na VOA kwa kubofya hapa.
Kusikiliza mahojiano hayo bofya hapa. http://www.voaswahili.com/archive/matukio-afrika/latest/2773/3100.html

No comments: